Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, March 18, 2009
HUU NI UZANDIKI

KITENDO cha wakubwa kujilipa bonasi ya $165 billioni wakati wamekomba fedha ya serikali $ 170 billioni ni fedheha na aibu katika ulimwengu unaomilikiwa na soko. Dhana ya kuwaacha wenye nguvu washike mpini kama walivyokuwa wakiachiwa na Bush haina haja kupingwa kwa nguvu zote. Hili ndilo linalotakiwa kufanyika hata kwa serikali maskini na sio kutazama tu watu wenye fedha nyingi wanajitoza kodi kwa kutumia mbinu za misaada huku wakinufaika na kutokatwa kodi kwa kigezo kuwa wanashiriki shughuli za umma. Obama anaonyesha njia sahihi katika hili pia. Habari zaidi soma hapa na pichani ni Treasury Secretary Timothy Geithner
 
© boniphace Tarehe 3/18/2009 12:16:00 AM | Permalink |


Comments: 6


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved