Sunday, March 22, 2009
HII NDIYO SURA HALISI YA AFRIKA
AFRIKA ni bara linaloongoza kwa kuwa na sura za umaskini hasa ule unaowafanya binadamu kukosa kile alichokiita Abraham Maslow haki za msingi yaani chakula, malazi na mavazi. Nimepita hapa na kukuta taarifa na picha hii ambayo kwangu haijanifurahisha.
Haki chakula ni jambo ambalo nimekuwa nikilizungumza sana na ninatamai siku moja kila mwananchi kwa kuanza na Tanzania apate haki hii ya msingi. Kama tukikubali kurejesha sera za vitendo katika kilimo bila shaka tutamudu kuwezesha watu wetu kupata chakula wakati wote.
tunafahamu kuwa wakishapata chakula kiasi cha kushiba ni jukumu la pili kusisitiza juu ya chakula bora. Wimbo wa chakula bra hauwezi sasa kuimbw ana serikali yetu kwa kuwa hata haki ya chakula tu kwa wananchi bado ni kitendawili. Kuna waziri wa Kilimo nchini anaitwa Wassira, ni maarufu sana kwa maneno matamu lakini utendaji wa wizara hiyo katika kutibu tatizo la upatikanaji wa chakula bado ni ndoto takayohukua siku nyingi kupata jibu. Tunasubiri sijui aje nani ili kuhamaisha kilimo cha chakula katika Afrika? Inakera na kuumiza sana!
© boniphace Tarehe 3/22/2009 07:21:00 AM


|
Permalink |
-
Kwa kweli naungana mkono nawe inasikitisha sana kuona hii picha. Na ni kweli chakula, mavazi , malazi na bila kusahau maji ni vitu muhimu sana kwa kila binadamu. Nimepita kukusalimia nawe karibu kijiweni kwangu ubadili mawazo.
-
Du! huyu kweli ana njaa. anafaa kusaidiwa kwani hata nguvu ya kulima huyu hana.
-
Jamani hii si njaa ni maisha magumu na umri wa kazi ngumu kwa maisha yote aliyoishi duniani, kwa kweli inasikitisha, haya ndiyo maisha ya wengi katika nchi za Afrika hususani katika nchi ya Wadanganyika kama TZ,Duu kamanda naona nimekumis sana katika Uga wetu ule tuliouzoea enzi zile, Uga wa MALENGA, naona kitabu kilikubana sana.
-
Tatizo la Tanzania ni kelele nyingi pasipo utekelezaji. Tangu tusikie kilimo kwanza mpaka sasa hatujui hasa mpango mzima wa kilimo kwanza unaanzia wapi na kuishia wapi au wimbo wa wanasiasa wa kutafutia kura kama siyo kula.
Nimesoma taarifa ya BOT kuhusu hali ya uchumi hifadhi ya chakula iko chini ya nusu ya hifadhi za vipindi vilivyotangulia. Tunaweza kujidanganya kwamba tunakaribia mavuno lakini kilimo hiki cha kutegemea mvua hizi na jembe lile sidhani kama kuna kitu cha kututia matumaini
Bibi kama huyu anahangaika kijijini kwa sababu tu hatakuwa na mtu wa kumlea, wote wamekuja tubanane mjiji kwani maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa ndoto vin=jijini
-
-
Kwa kweli naungana mkono nawe inasikitisha sana kuona hii picha. Na ni kweli chakula, mavazi , malazi na bila kusahau maji ni vitu muhimu sana kwa kila binadamu. Nimepita kukusalimia nawe karibu kijiweni kwangu ubadili mawazo.