NI siku nyingi sijaingia hapa, wengi wamehoji haka kaukimya nimekaanzishia wapi. Nikajiuliza tena binafsi nimelala wapi? Lakini kuna kubwa moja, ukimya una mafunzo makubwa na unamkuza mtu akitaka kufanya tafakari. Nikionacho katika maisha yangu ni furaha, nawatazama watu wengi wakianza kuishi furaha hii. Wengi niliwapoteza lakini sasa wanaanza kurejea kwa kasi mno.
Maisha yangu yanakuwa huru kiasi, nakosa makundi ambayo yalianza kujijenga. Lakini kuna ndoto zinazoingia na kutoweka. Moja ni hii ya siasa! Siasa jambo baya maana lahusisha mbinu mbaya na chafu. Kuna kundi limeingiza mbinu zisizoonekana katika kuweka mambo sawa katika siasa, lakini binafsi naamini sasa katika siasa elimu.
Nina jukumu mbele yangu na hii ni safari ya kutafuta PHD nikiifanikisha safari hii nitafarijika sana. Nitafurahisha moyo wangu maana ni jambo ambalo nimekuwa nikilipenda sana na hata Mzee Benjamin Makene amekuwa akishangilia kuhusu wazo hili. Najua nitakuwa na jukumu la familia maana mimi si kiumbe wa kuwepo kuwepo tu. Nitalizungumzia hili siku zijazo maana hapa ndio kasrini kwangu, ambapo sasa pia panachapishwa katika gazeti la Rai na nategemea hata nyumba yangu kuwa na jina hili. Nishukuru kurejea kwa staili hii, nijipe moyo maana kuwepo na kuondoka zote ni faraja na mikakati ya Jalia.
Good Luck with that Bro. Natambua kuwa unaweza maana nakufahamu ama niseme nakumbuka saana jinsi ulivyokuwa uki-execute malengo yako kule Sec. Wakumbuka enzi za "over-lakers" ndani ya Ihungo?
Haya tuko pamoja na nakuombea kila lililo jema si kufanikisha na kumfurahisha mzazi, bali pia jamii ambayo umeitumikia vema na itanufaika zaidi na zaidi.
Blessings