Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, November 23, 2007
NIPO
KATIKA harakati za kutoka kuzimu mimi Boniphace Makene natangaza kurejea duniani humu. Safari yangu ya kuzimu ilikuwa ndefu na hadi narejea hapa nina uchovu mwingi. Sitarajii kuwa kuzimu karibuni lakini nimejifunza mengi katika safari yangu hiyo.

Nimejifunza kuhusu kuingia zama mpya ambazo zinaweza kuwa hatari kwa maisha ya watu wengi. Nimejifunza utamaduni mpya wa watu kuvuana nguo bila kupenda. Nimejifunza na kujifunza na taarifa nyingi nitazungumza nanyi siku zijazo.

Nitumie fursa hi kuomba radhi kwa wale ambao sikuwaaga wakati nachukua maamuzi ya kusafiri safari hiyo. Nimerejea ndugu zangu na kama niko salama nadhani mnaweza kuona. Niishie hapa maana bado nina uchovu. Karibuni katika Kasri lenu ambalo mmelitunza hata wakati nikiwa safarini.
 
© boniphace Tarehe 11/23/2007 11:41:00 PM | Permalink |


Comments: 2


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved