Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, November 22, 2006
Baadhi ya safari za Rais Jakaya Mrisho Kikwete nje ya nchi
HIZI ni baadhi ya safari za Rais wa Tanzania, bado sijaweka sawa kuhusu zile za Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wake. Zitazame na kisha changia kwa ufahamu wako kuhusu faida na atthari zake. Kumbuka Rais na serikali yake hawajamaliza hata mwaka mmoja wakiwa madarakani.

Januari 19-25, 2006 – Khartoum, Sudan kuhudhuria mkutano wa AU
Machi 23, 2006- Ziara ya siku moja ya kiserikali kujitambulisha Kigali, Rwanda.
Machi 22, 2006- Ziara ya siku moja kujitambulisha Kampala, Uganda.
Machi 24, 2006 Ziara ya kiserikali kujitambulisha Nairobi, Kenya.
Aprili 19-20, 2006 Ziara ya kujitambulisha Lesotho na Swaziland.
Aprili 21-22 , 2006 Ziara ya kujitambulisha Maputo, Msumbiji.
Aprili 28, 2006 - Ziara ya kujitambulisha Harare na Bulawayo, Zimbabwe.
Aprili 6, 2006 – Ziara ya kujitambulisha Gaborone, Botswana.
Aprili 10-12, 2006- Ziara ya kujitambulisha Widhoek, Namibia.
Aprili 7-9, 2006 Ziara ya kikazi na kujitambulisha Pretoria, Afrika Kusini.
Mei 12,2006 - Ziara ya kiserikali ya wiki mbili kwenda Uganda ambako alikaa Mei 13, Arabuni Mei 15, Ufaransa Mei 16-19 na Marekani Mei 21-26.
Mei 31-Juni 3- Ziara ya kuhudhuria World Economic Forum, Capetown Afrika Kusini.
Julai 4- 2006- kuhudhuria mkutano wa AU,Banjul Gambia
Julai 10-32, 2006 Capetown Afrika Kusini , kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali ulioandaliwa na kampuni ya Microsoft ya Marekani.
Julai 20 – Kuhudhuria mkutano wa Leon Sullivan Summit Abuja, Nigeria.

Julai 21 -22, 2006 – kuchunguzwa afya Berlin Ujerumani.
Agosti 19-20- Kuhudhuria mkutano wa SADC, Maseru, Lesotho.
Agosti 21-22- Ziara ya kiserikali Luanda, Angola.
Septemba 12- Havana Cuba maandalizi ya kikao cha NAM
Septemba 15, 2006 Alipita Madrid, Hispania kwenye Uwanja wa Mpira- Real Madrid.
Septemba 15 -18, 2006 Havana Cuba, Mkutano wa NAM.
Septemba 19-25 - Kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
© boniphace Tarehe 11/22/2006 09:17:00 PM | Permalink |


Comments: 11


  • Tarehe 11/22/2006 10:45 PM, Mtoa Maoni: Blogger bongozite

    Hizi ziara zote pia zinasaidia sana kupromote Tanzania. Magazeti ya nje yataandika kuhusu Tanzania na ziara ya raisi. Wafanya biashara ambao wanaweza kuekeza na kuona opportunities watakimbilia Tanzania. Touarism inapata promotion moja kubwa sana. Tanzania inajulikana kwa umasikini sasa ziara za raisi zianondoa hiyo na kuionyesha tanzania kama ni nchi ya uwezekano, maendeleo na nchi nzuri ya mapumziko.

     
  • Tarehe 11/25/2006 1:56 AM, Mtoa Maoni: Blogger Unknown

    sielewi vizuri protocol za SADC naona nchi nyingi rais alizoenda kujitambulisha ni SADC na east africa.kitu ambacho kinasikitisha katika safari hizo na za viongozi wetu ni safari za kwenda kuangalia afya zao nje!!!ni nini wanachokifuata kwenye hospitali za nje ambacho wameshindwa kukiweka kwenye hospitali zetu???haya ni madhara ya kutojua tu na pamoja na kasumba,na inakera tena inakera sana.kwa gharama ndogo kuliko za viongozi wote wanaoenda kutibiwa nje kwa mwaka tungeboresha hospitali angaliau moja na ingetibia watanzania wengi zaidi!ee mwenyezi mungu wafungue macho viongozi wetu na wajalie moyo wa huruma.

     
  • Tarehe 11/25/2006 9:06 PM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Afanaaleik huyu ndiye Rais tuliyempa kura zetu ameamua kuwa mtalii ilhali wapika kula wake wakiendelea kufa njaa kukosa tiba ya uhakika na baadhi ya akina mama wajawazito wakifa kwa kukosa huduma za uzazi, mie sisemi nikisema nitaambiwa oooh napinga sera za chama twawala za Ari Mpya Nguvu Mpya na Kasi Mpya bila fikra mpya.

     
  • Tarehe 11/26/2006 11:07 PM, Mtoa Maoni: Blogger mnyalu

    Asante sana bwana Makene kwa kuona mbali.

    Unajua nimeshaona watz wengi bado hawajajua swala la 'Opportunity cost'. Hivi unawezaje kulipa kipaumbele swala la safari nje ya nje ukiwa rais, kuliko kukaa na viongozi wa ndani na wananchi kutafuta suluhu ya baadhi ya matatizo yanayotatulika. Safari siyo kitu kibaya, lakini kipindi hiki ni kigumu kiuchumi na hata kwa miundo mbinu na nishati katika Tanzania. Nahisi kama rais na baadhi ya wanaozikubali hizo safari, hawaonji shida ya Watanzania iliyopo sasa.
    Kibaya zaidi safari anazofanya rais, kama za kutangaza mazingira ya biashara nk, zinaweza kufanywa na waziri Migiro. Au yeye mheshimiwa rais hajajua kuwa yeye ni rais sasa, na si waziri wa mambo ya nje? Shida ya misafara ya rais ni kwamba inagharimu pesa nyingi sana kuliko angemtuma waziri wake. Sababu moja ni msafara wake mkubwa anaofuatana, acha familia yake kama mke na watoto, kuna msululu mkubwa wa wafanya biashara, wanasiasa na viongozi toka ofisi yake.
    Nchi kuwa na amazingira mazuri ya uwekezaji hakutangazwi kwa safari tu. Bali ni kuandaa mazingira mazuri. Wenyewe tu wataambizana kuwa Tanzania kunafaa. Kwa taarifa, mataifa ya magharibi na Marekani, yanajua kilichomo ndani ya TZ hata kabla raisa hajasafiri kuwaeleza kuna nini. Wenzetu wanathamini sana habari 'Information is Power' kwao. Hivo wana habari zote za Tanzania, hata kama saa zingine huamua kuzipotosha kwa maslahi yao.
    Nadhani rais amekuwa na malengo mengi mno kwa mpigo. Anahisi kila kitu kinaweza kufanyika mara moja namna hiyo. Saa zingine hata nikisikiliza hotuba zake namwona kama shekhe au askofu na waumini wake. Maana anaweza kuongelea tatizo na kuwapa matumaini hata kwa swala ambalo hajui utatuzi wake unawezekana au la.
    Sasa rais akiwa mhubiri, raia wanajua kuna kitu hapo? Uzuri alionao ni kwamba anakubalika na watz wengi. Na wengi wao ukiwauliza kwanini wanadhani aanafanya kazi nzuri, hawajui. Ni kama tu kufuata upepo. Kuwa na uchungu na matatizo ya watz peke yake bila kuwa na utatuzi ni kama haisaidii kitu. Namwunga mkono Tegembwage pia, aliyeonya vyombo vya habari kutosifia kazi zinazofanywa na serikali, kwani wanatimiza wajibu wao. Hii inaonesha kuwa tumezoea kuwa na viongozi ,atapeli, kiasi tukipata mtu asiyemwongo, tunajiona tuna bahati, wakati ni haki yetu kuetendewa hayo wanayotenda kama kutimiza ahadi zao.

    Naweza kuongea hadi kesho kwani yapo mengi yanayonikera ila sioni kama Tz ni nchi ya kuibadisha siku moja. Ila tunakokwenda hili tabaka litakuja tu kung'olewa. Hata dola imara kama ua Kirumi, Uingereza na zingine, nani alijua kuna siku zitakuja kuwa chini? Ngoja tu muda tutakuja kuona mabadiliko, ni swala tu la muda. Nashukuru wengi sasa wanasoma Tz.

    Mwisho, bwana Makene, hizo safari ulizotaja ni badhi tu ya zile alizofanya rais nje ya Tanzania. Mbona sijaona umetaja nchi yoyote ya mashariki ya kati. Nakumbuka alishaenda sehemu kama Uarabuni Saudi na Mwungano wa Falme za Kiarabu (UAE), maeneo ya DUBAI.

    ASANTE......KEEP US INFORMED.

     
  • Tarehe 11/27/2006 7:55 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Sasa Makene hizi si ndio faida za Urais? Yaani hutaki naye atembeetembee? Akibaki nchini hapo umeme hakuna mnampigia makelele. Sasa lazima akajipumzishe pumzishe nje. Au?

     
  • Tarehe 11/29/2006 8:52 AM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    nimefurahi kukutana na wewe leo hapa dar. tutapoonana naona tutaongelea kwa kina safari hizi na zijazo. ila ndesamjo kanichana mbavu hahahaaa!!!

     
  • Tarehe 11/30/2006 10:57 PM, Mtoa Maoni: Blogger Christian Bwaya

    Mwacheni Rais atembee jamani? Kopo la "nisaidie baba" litatembezwa na nani akibaki nyumbani?

     
  • Tarehe 12/03/2006 3:58 AM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Bonny nimewahi kusoma sehemu fulani kuwa tuziara anatotufanya bwana mkubwa tumeanza kuzaa matunda. sasa sijui ni ileile maneno ya wanamtandao kufagilia na kusifia hata pakiwa pana uwongo. Si unawajua wanamtandao.

    Hivi ile enzi ya Nyerere ya kuwatuma mawaziri kwenda nje kwa shughuli hizi hizi haitarejeaga tena eti.

     
  • Tarehe 12/11/2006 1:51 PM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    bonny!

    hongera kwa kumbukumbu, ingawa sijakusamehe kwa kuingia mitini...

     
  • Tarehe 12/16/2006 5:14 AM, Mtoa Maoni: Blogger Sultan Tamba

    Kutembea tembea ndiyo staili aliyoingia nayo Mkuu wetu wa awamu ya nne. Au Mmesahau Mzee Mkapa alivyoingia alikuja na staili gani? Ntawakumbuka; yeye aliingia na mkwala wa kutoa hotuba bila kusoma kwenye makaratasi! Popote pale anabonga tu! Kama Nyerere! Matokeo yake akajikuta anakanusha maneno yake mwenyewe kwenye vyombo vya habari mara tano mfululizo! Magazeti yakamchora katuni, yakasema sasa rais wetu anakaribia kuingia kwenye kitabu cha Guinness kwa tabia yake ya kukanusha kanusha maneno yake! Kuanzia hapo akaacha! Kila hotuba, anasoma katika karatasi! Nna wasiwasi hata alipokuwa akialikwa kwenye bethdei akiambiwa atoe mawili matatu! Anafungua karatasi, anasoma!
    Na Kikwete ataacha tu! Msiwe na wasiwasi!!

     
  • Tarehe 6/13/2015 1:23 PM, Mtoa Maoni: Blogger imanauliya

   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved