Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, October 04, 2006
MSIMAMO WA KASRI KUHUSU NYUMBA ZA SERIKALI
NIMEONA nidokeze baada ya wana Kasri Kutaka kufahamu kama msimamo wetu kuhusu nyumba za serikali umebadilika baada ya Rais Kikwete kutangaza kuwa atarejesha baadhi ya nyumba zilizouzwa! Hapana, ndugu bado naamini Kikwete ana jukumu la kurejesha nyumba zote na kama ataona tabu basi zile zenye hadhi ya kuishia na vyeo vya kuu vya wilaya! Hapa nahusisha wakuu wa wilaya, wakurugezi wao na wengine hadi nafasi ya rais! Hawa watu wanaweza kujenga nyumba zao na nafasi zao zinawawezesha kupata viwanja popote watakapo hivyo warejeshe nyumba za umma! Zoezi zima la uuzaji lilinuka uchafu wa rushwa na pia lililenga kunufaisha watu kutokana na nafasi zao. Kunahitajika kurejesha nyumba hizo zote na kisha kuomba radhi umma kutokana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha waliohusika kushswishi tukio hili hasa wale walioanzisha hoja pale Leaders Club!

Rais bado msimamo wangu kuhusu nyumba sijaubadili nitafurahi kusikia siku umetanza kurejesha kwanza yako maana siku hiyo itakuwa ni nuru ya kufuata za wengine wakubwa! Mkumbuke Sokoine katika hili na ukimtazama sana unaweza kuanza kujikana wewe na kufungua safari hii. Kumbuka raia maskini tuko nyuma yako katika hoja hii na hakuna kigogo wa kuweza kukudhuru baada ya kutimiza kero hii inayobaki vichwani mwetu siku hadi siku.
 
© boniphace Tarehe 10/04/2006 12:01:00 AM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 10/07/2006 4:32 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Makene, kuna makala kali sana uliandika huko nyuma kuhusu hili suala. Tuwekee kiungo hapa kutukumbusha uliyosema wakati ule ambapo naona kuwa msimamo wako ni ule ule. Nakubaliana nawe. Watu wenye uwezo wa kujenga nyumba zao, tena zaidi ya moja, bado wana tamaa ya kutwaa nyumba hizi za umma.

     
  • Tarehe 10/09/2006 4:14 AM, Mtoa Maoni: Blogger mzee wa mshitu

    kaka huu msimamo ni makini sana na kama unavyosema zirudishwe sisi wana kasri tunataka spade iitwe spade siyo mara unasema koleo, mara beleshi mata nini sijui. Tunataka nyumba za umma zirejeshwe.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved