Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, October 15, 2006
HAPIBETHIDEI KASRILAMWANAZUO
TAREHE rasmi ya kuzaliwa gazeti Tando la Kasrilamwanazuo ni hii leo Oktoba 15. Lilianza awali na kisha maandishi ya kwanza kupotea. Hali hii ilitokana na uduni wa taaluma ya teknolojia hii. Kuna wengi naweza kuwashukuru kuweza kunipa mwanga wa kuweza kuingia katika mapambano haya ya fikra na uwezo wa kumiliki eneo langu na kulilima na kulipalilia nipendavyo huku nikitoa fursa kwa wavunaji kuvuna wapendavyo lakini kwa staha!

Nilipokuwa DARUSO kama Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi nilipata changamoto kubwa, hatukuweza kuwa na mtndao wetu kwa kile kinachozungumzwa ukosefu wa fedha za kuuendesha. Dhana yetu ilikuwa kusaka malipo kwa watakaoandika na watakaoutunza mtandao huo. Lakini msemo wa kidole kimoja hakivunji chawa mbona unapata sulba kutokana na kutofaa hasa mimi ninapoweza kumiliki Gazeti Tando na kuliwekea taarifa mara kwa mara wakati pale chuoni wanafunzi wote ambao ni wanachama wa DARUSO kwa sifa ya uanafunzi wao wanashindwa kumiliki mtandao wa kuweka taarifa za chama chao?

Nitapita hapo chuoni siku zijazo kujadili suala hili na ikiwezekana kuanza kuvua wanavyuo mbalimbali kuingia katika ukurasa huu wa kutunza kumbukumbu zao kwa ajili yao na jamii inayowazunguka.

Katika mwaka huu mmoja nilioutimiza nina mengi ya kufafanua lakini kubwa ni kushindwa kufanikisha matakwa ya wasomaji wangu hali inayonifanya kuwaza sasa kutanua ukurasa na kufungua kitu kingine kipya siku zijazo. Kuna wengi wanalilia kukosa maji ya kunywa lakini mimi nalia na ukame wa mawazo katika ukuzaji wa fikra na mtazamo wangu na jamii yangu. Ninaamini Afrika ni taifa chimbuko la mtu mweusi na ni sehemu hiyo pekee mtu huyu atapata faraja ya kujivunia kama akipenda. Ninaamini kila sera inayotangaza kuungana kwa watu maana sishabikii utengano! Nachukia wanaotumia muungano kuneemesha ubinafsi wao na kikubwa nawachukia viongozi wa Afrika wasio na mtazamo kuwa Afrika inaweza kusimama yenyewe na ikatembea bila kujipendekeza kusaka misaada na mikopo inayodhalilisha utu wetu na kisha kuliweka rehani bara letu tukufu.

Naomba nisihutubu sasa nimezaliwa na ninatembea kama hujathibitisha soma utangulizi wa hutba hii katika utungo ulio hapo chini. Nikusalimu Mama yangu Esther Makene "Mama Tazama mwanao" Nikuamkue kaka Mwalimu Benjamin Makene, "Komredi msalimu Mwalimu Mwenzio Nyerere, nakuamkua Mzee Mwalimu Benard Makene, "Unyonge wetu ndio kikwazo cha kufanikiwa kwetu, tusiukumbatie!" Nimalize na wanazuoni wote "Hakuna chakula bora kupata kupatikana katika milki zote za dunia kama fikra! Kuleni fikra mtajaza ulimwengu wenye weledi na wenye vipaji razini.

Mwenyezi Mola tazama na bariki kazi za mwanao!

Komredi Boniphace Makene
 
© boniphace Tarehe 10/15/2006 02:16:00 AM | Permalink |


Comments: 18


  • Tarehe 10/15/2006 3:44 AM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

    Kaka hongera sana kwani ni jambo la kheri kichwa kimoja cha zuoni kikitimiza kipindi flani cha uhai katika uzandiki wa maneno machafu yanayowekwa na watu wasio na majina.Hepibethdei kaka

     
  • Tarehe 10/16/2006 6:36 AM, Mtoa Maoni: Blogger mzee wa mshitu

    Kaka hongera happy birthday Kasri happy birthday fikra tunafurahi saaana sisi tupendao chakula hiki cha aina yake fikra ni chakula muhimu kama unavyosema.
    Usidhani kwamba umeshindwa, nikuambie kitu kimoja umeshinda kwa kiasi kikubwa kutujaza fikra mpya na pana zaidi.
    Naomba ndoto zako za kuwapelekea wazo la kuingia mtandaoni vijana wa pale mlimani litekelezeke ili kusudi tuwe na uwanda mpana zaidi.

     
  • Tarehe 10/16/2006 3:30 PM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    Komredi Makene hongera!

    Ama kweli siku zayeyuka, yaani ni kama jana tu umeanza kujenga hili kasri, ambalo mada zake zakuna vichwa vya walio na wasio wanazuoni. Happy Birthday and may the Kasri live to be a 1000 years!!!

     
  • Tarehe 10/17/2006 12:05 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Heri ya siku ya kuzaliwa.Wewe ni mhimili,tafadhali endelea kusimama ili nasi tusianguke.

     
  • Tarehe 10/17/2006 12:05 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Heri ya siku ya kuzaliwa.Wewe ni mhimili,tafadhali endelea kusimama ili nasi tusianguke.

     
  • Tarehe 10/19/2006 3:38 AM, Mtoa Maoni: Blogger Egidio Ndabagoye

    Nimechelewa kupita Kasirini kaka sababu ya pilikapilika za huku Ughaibuni.Happy birtday Kasri

     
  • Tarehe 10/19/2006 12:54 PM, Mtoa Maoni: Blogger MTANZANIA.

    Hongera Makene kwa kulifufua kasri la mwanazuo.

     
  • Tarehe 10/20/2006 4:54 AM, Mtoa Maoni: Blogger Simon Kitururu

    Hongera nyingi zikufikie!

     
  • Tarehe 10/21/2006 8:08 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

    Hongera. Endelea kaka.

     
  • Tarehe 10/24/2006 5:50 AM, Mtoa Maoni: Blogger Deus Ngowi

    Kasri limejengwa likajengeka,
    Limepambwa na likapambika,
    Tungie ili tuweze kujengeka,
    fikra zetu tutoe, ifaidi Afrika.

    Kila la kheri, na nawapa wote mkono wa Idd.

     
  • Tarehe 10/27/2006 4:45 AM, Mtoa Maoni: Blogger MK

    Ongera sana ndugu kwa kutimiza mwaka mmoja.

     
  • Tarehe 10/28/2006 2:38 AM, Mtoa Maoni: Blogger Unknown

    hongera sana comrade.kumbe hili kasri limezaliwa tarehe sawa na mimi!!!

     
  • Tarehe 10/29/2006 3:24 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Kasri, pongezi zote zikujie kwa kutimiza mwaka toka ukate shauri na kuanza kutupa vipande, mashairi, makala, na changamoto za kila aina kupitia kasrini. Tupo pamoja. Mbele kwa mbele. Kama ulivyozoea kusema (natumia maneno yangu), "cheza karata yako...."

     
  • Tarehe 10/29/2006 3:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Ajabu kanisa Makene kuona wanafunzi wa vyuo hawaonyeshi ubunifu wa kutumia teknolojia ambazo sisi tunazitumia bila kizuizi chochote. Huenda walimu pale wanawadanganya badala ya kuwafundisha au kuwasaidia wajifunze. Huenda ndio maana Bob Marley akasema, "Dont let them fool you, or even try to school you" alijua mfumo wa elimu unaweza usiwe ndio nyenzo ya kumkomboa mwanadamu na kumpa zana na maarifa ya kupambana na mazingira yake. Sababu hii ndio ilinifanya nikachukia shule (sio elimu na maarifa) toka nikiwa madarasa ya chini kabisa. Nilishtuka kama alivyoshtuka Fela na kuimba, "Teacher dont teach me nonsense!"

    Haya, hongera tena kwa kuzaliwa.

     
  • Tarehe 11/09/2006 8:19 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rundugai

    Hongera sana kwa kutimiza mwaka japo nimechelewa kuingia kasrini lakini tupo wote kwa makala yako kila Jumapili kupitia mwananchi Jumapili.Keep it up

     
  • Tarehe 11/11/2006 3:31 AM, Mtoa Maoni: Blogger Mija Shija Sayi

    Makene, Watanzania tuna bahati ya kuwa na mtu kama wewe. Na hapo bado unasema una ukame wa mawazo na fikra!!

    Hongera kwa kutimiza mwaka.

     
  • Tarehe 11/13/2006 3:26 AM, Mtoa Maoni: Blogger Christian Bwaya

    Hongera kaka kwa kuzaliwa. Endelea kucheza karata yako.

     
  • Tarehe 11/22/2006 3:09 AM, Mtoa Maoni: Blogger mloyi

    Unakuwa mkubwa na kusahau kusimama?
    Ukubwa gani huo? Tunakosa mambo ya kasrini.
    Hongera.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved