Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, July 18, 2006
SIJALALA BADO!
SIJALALA hata kidogo, macho yangu makavu kabisa natazama huku na huko. Namuona rafiki yangu anageuka adui, na si adui kabisa maana neno hili lina maana hasi kidogo! Anageuka shetani, anachukua kila aina ya silaha kutaka kuniangamiza! Namuoana hanionei hata huruma tena na sijui nani kamfanya hivi!

Natazama kushoto naiona familia yangu ikilia inanitazam kwa uchungu lakini yote imefungwa kamba na kuzibwa midomo! Nawaona mke na wanangu wakiwa na majeraha makubwa katika miili yao. Wnalia na kilio chao kinanipa maumivu makubwa kuliko haya ambayo nimekuwa nayo kwa usiku huu mzima wa vipigo ambavyo mwanzo wake siutambui!

Natazama walionizunguka ni hawa ambao walicheka sana na mimi na wakibadili hulka nami kila mara! Nawatazama wanapoona hata raha kutaka kuwa na nafasi ya maamuzi ya mwisho kuhusu maisha yangu! Ghafla nguvu zinanitokea nakata kamba zote na kuwaangusha hawa adui zangu chini. Wanahaa kutaka kujiokoa maana wanadhani mimi nitalipiza kisasi. Nawatazama kwa dharau na kisha nawafungua wanangu na mke wangu na kisha nawapaka divai katika majeraha yao. Nikisha maliza naondoka bila hata kujali kuwa adui zangu bado wana mitutu wanataka kunitungua kisogoni! Nimejawa nguvu sana, sioni maumivu na mwisho nawakaribisha kahawa na kashata adui hao ili wajumuike nami kama watu wa muhimu kabisa kuchangia mafanikio ya maisha yangu!

Ninapoaamka nacheka na kukumbuka maana ya maono haya. nAMTAZAMA RAFIKI YANGU AMBAYE SIKU ZOTE AMEKUWA RAFIKI KWELI. nAMTAZAMA YULE ALIYEAMUA KUASI NA KUWA ADUI NA HAISHI KUSIMULIA UZOEFU WAKE WA KUWA NA MIMI KATIKA MAISHA. nATAZAMA HUYU KWA JICHO LA KEBEHI KIDOGO. Kisha, nakumbuka kuwa majira ya joto yanaisha na ubaridi utaanza na kisha siku zitaendelea. Nakumbuka kuwa nitakapolala usingizi watakaofahamu kuwa nimekufa ni familia yangu tu na umma mwingine utabaini kuwa nimelala. Najua tena kuwa ni mke na wanangu watakaoziba kauli zao kuhusu mimi lakini maadui na hao waliojisingizia rafiki zangu watakaopaza kauli za sifa kali kali kwangu! Ninazitaka hizi kweli, zinanifaa hizi kweli, aaaah si bora niamke nianze safari ya kutafuta mhogo na kshata kwa ajili ya chakula cha asubuhi!
 
© boniphace Tarehe 7/18/2006 08:04:00 AM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 8/12/2006 4:31 PM, Mtoa Maoni: Blogger cyborgafrika

  This comment has been removed by a blog administrator.

   
 • Tarehe 8/31/2006 5:39 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

  Du!!! mzee hii ni fasihi simulizi?ni ndoto au ni nini maana nimesoma nimegundua kuwa una hazina kubwa ya fikra kwa watu wa zama zetu hizi kwani si aghlabu kuwepo watu wenye fikra za kifasihi aina hii, mara nyingi yaliyopo katika jamii hushabihiana na maono yako na hii ndiyo hali halisi iliyojengeka kati ya mtu na mtu binadamu amekuwa adui wa binadamu mwenzie ilhali wanyama wa namna moja hawana uadui mingoni mwao.

  Hii ni zahama katika dunia iliyojivika gunia bovu.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved