KILA siku maana ya magazeti tando inatanuka. Wengine wanaamua kuyatumia kama njia ya kuwasiliana nandugu na jamaa zao na kubadilishana picha, mawazo na maoni. Wengine wanayageuza kuwa sehemu za kutunzia kumbukumbu. Ndugu yangu
Juma Kitenge yeye kaamua kuwekan picha za matukio yake na wengine katika ukumbi wake na hii itampa fursa kuwa karibu na ndugu na jamaa zake wa karibu waliko kote ulimwenguni. Waweza kupita hapo na kutazama nini alichoweka maana kama ujuavyo binadamu twajifunza kutoka kwa wengine, unaweza kuwa wafahamu watu huko, kwako Baragumu ambaye bado unatafuta!