Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, June 27, 2006
OOOHOOO UMEMUONA MWINYIMBEGU?
HATUJALALA kama ambavyo jamaa fulani wanadhani, tumeamua kuchukua tathimini hasa baada ya timu zetu kubanjuliwa nje ya michuano ya soka ya Dunia. Je kuna haja ya Afrika kuwa na timu tano au tuzipunguze kabisa na au tusiwe na hata moja? Nitajadili uwanja huu siku nyingine lakini leo nimtambulishe kwenu huyu mwanaharakati aliyekuja kwa namna yake. Pita kwake msalimu mtazame na kisha utabaini kasi ya magazeti tando inavyozidi kuchana anga. Karibu Mwinyimbegu na waungwana watabonyeza hapa na kukusalimia huko.
 
© boniphace Tarehe 6/27/2006 10:01:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 7/04/2006 7:01 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Makene, shukrani kwa kutupasha habari hii njema ya ujio wa Mwinyimbegu.

     
  • Tarehe 7/07/2006 4:51 AM, Mtoa Maoni: Blogger SIMON KITURURU

    Mimi nahisi kinamna fulani tumelala.Mimi nahisi katika sehemu ambazo Afrika tunaweza ku fight back ni katika kabumbu. NA mapigano hayo yanatakiwa yawe katika hali ya juu kuliko wao. Nakumbuka Hoja ya sidney Poitier akizungumzia nini kilikuwa kinampa ari ya kwenda kazini hapo hollywood kipindi ambapo mweusi alikuwa pekee mpaka ikabidi tu wampe Academy award(Oscar). Alisema kuwa ilibidi yeye afanye vizuri mpaka kusiwe na mtu ambaye anaweza akatoa hoja ya kukubalika kuhusu uwezo wake wa kuigiza. Sasa hivi timu za Afrika bado hatujafikia kufuta hoja kuwa kweli tuna jua mpira kwa sababu tunafungwa. hata game ya Ghana na Brazil kwamtazamo wangu Ghana ilicheza vizuri kuliko Brazili lakini huwezi kukataa kuwa ilifungwa.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved