Wednesday, May 03, 2006
SHUKRANI WAZIRI MK
NDUGU zangu mnaotembea hapa msinituhumu kwa wizi wa mali ya umma katika kujenga jengo hili jipya. Ukweli kilichotimia hapa ni kile kiliwahi kuzungumzwa na walii mmoja aliyesema, "mmepewa bure nanyi toeni bure." Komredi waziri wetu wa Teknolojia katika jamii ya wamiliki wa magazeti tando afahamikaye kama MK amejenga nyumba hii bure kabisa. Sijalipa chochote na bado anafanya matengenezo zaidi hivyo haijakamilika.
Kama nawe wapenda kufanyika haya kwa nini usimtafute MK ili aweze kujenga nyumba yako. Kwa kweli Tanzania tuna watu wetu waliojaliwa mengi, MK nakushukuru sana na kukuomba kuboresha nyumba za watanzania ili zitishe kuliko hata hawa wanaotokea mataifa makubwa.
© boniphace Tarehe 5/03/2006 05:27:00 PM
|
Permalink |
-
Ni kweli ndugu yangu hii hatua ya Waziri wetu MK inapaswa kupongezwa maana imetuondolea uzungu wote katika blogu zetu na sasa tumekuwa na touch ya kiswahili, kwani ni wachache sana wenye vipaji na moyo kama yeye ingekuwa wengine wangelikaa kimya.
-
Imekuwa nzuri, ingawa ilinisumbua kidogo kujua nikutembelee vyumbani kwako kupitia njia ipi. inapendeza, inanitamanisha na mimi pia nimuite waziri Mkuu kwenye nyumba yangu.
-
Nyumba imetulia..safi sana Makene na pongezi pia kwa MK.
-
MK nakuvulia kofia sio tu kwa kurembesha nyumba hizi za majirani zetu bali pia, tena hasa, kujitolea kutoka muda wako, ambao nashawishika kuwa ni mdogo. Hongera thana (kipare-pare) Jeff upo!
-
Nashukuru ndugu zangu wote kwa kunipa pongezi hizi.
Muda huu uwa naupata nikiwa kazini au nyumbani kama sina kazi nyingi za kufanya, Vile vile inatokana na sababu ya kwamba ninapenda sana Computers hivyo basi furaha yangu inakuwapo (Inazidi) nikiwa ktk computer nikifanya kazi mbali mbali.
Nashukuru sana ndugu zangu.
©2006 MK
-
Makene makazi mapya yanavutia nimefurahia kuwa humu ndani, na kuondoka inakuwa ngumu. Pongezi sana kwako na kwa mjenzi, MK.
Ukweli ni kwamba kama anvyosema Mwaipopo, kazi hii ya kujitolea kufanya vitu vikubwa hivi inastahili kupongezwa.
Ngoja niendelee kutembea tembea kuona madirisha na kuta za nyumba hii....aisee!
-
Mimi nimeshampongeza MK mara nyingi sana na sijakoma. bado naendelea. Kama utakumbuka makene, nilimeshambatiza kuwa ni zaidi ya John Magufuli, anajenga nyumba anagawa bure, anajenga anagawa bure hadi kila mtu awe na Jumba la kisasa.
-
Nampongeza sana MK kwa moyo wake huo, nami nitaomba ushauri mwingi toka kwake. Nampongeza pia Ndesanjo kwani ndiye aliyenifungua macho. Hongera.
Ni kweli ndugu yangu hii hatua ya Waziri wetu MK inapaswa kupongezwa maana imetuondolea uzungu wote katika blogu zetu na sasa tumekuwa na touch ya kiswahili, kwani ni wachache sana wenye vipaji na moyo kama yeye ingekuwa wengine wangelikaa kimya.