Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, April 25, 2006
WATANZANIA PENDANENI NA KUTHAMINIANA-KIKWETE
Nilipokea mail hii kutoka mtandao wa Jumuiya ya Watanzania waishio Houston Texas, Marekani. Hii ni jumuiya inayokuwa kwa kasi sana na kufahamu majukumu yake kwa wananchi wa Tanzania. Mungu awabariki sana wanajumuiya hii kwa moyo wenu wa ukarimu, upendo na kusahau yanayopita!
Basi wiki zilizopita Rais Kikwete aliwataka Watanzania walioko nje na hasa wanaopata nafasi za kazi kutoa taarifa kwa watanzania wenzao walioko nyumbani ili wazichangamkie. Nichukue fursa hii kukupongeza James Magwe wa Houston kwa kukubali kauli ya Rais wetu na kuanza kuitekeleza kama ujumbe wako usemavyo, nakunukuu kabisa:
"Napenda kutoa mchango wangu kutimiza aliyosema Mhe. Rais Kikwete.. hii hapa ni website ya UN kwa maswala ya kazi http://jobs.un.org
Watanzania mnakaribishwa kujaribu kutafuta kazi kwenye UN System.. zipo nyingi na zinapatikana"


Haya shime watanzania, waafrika na wengine mnaofika Kasirini, changamkieni kazi hizi ili muitumikie dunia hii na kujenga nchi yetu na bara letu. Waweza kubonyeza moja kwa moja hapa pia.
 
© boniphace Tarehe 4/25/2006 06:05:00 PM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 4/26/2006 8:06 AM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Makene,

  Mbona hata hapa bongo dili ni hiyo hiyo, matangazo kibao ya ajira, lakini hebu chunguza ni nani anaingia ofisini. Nadhani alichokisema au kukisisitiza ni kuvutana wenyewe kwa wenyewe kwa maana ya kurahisisha kazi ya kuingia ofisini.

  Nadhani pia unakumbuka Januari nilipokuwa huko, nilipokuwa pale Umoja wa Mataifa, haki ya Mungu unaweza kushangaa Wanyarwanda na Warundi kibao, Halafu kiswahili kinachozungumzwa pale ni cha Wakenya na Wacongo DRC. Watanzania ni kama vile hatupo.

  Kuanzia getini ukizungumza kiswahili unasikia mtu lazima atakuita au kukujibu na utakapozungumza naye atakweleza kuwa ni Mkenya sasa sisi kwani hatuwezi hayo?

   
 • Tarehe 4/27/2006 6:55 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Makene,
  Napitia muswada. Kalamu yako inamwaga wino hasa!
  Tafadhali mtumie pia Freddy Macha. Ni mchambuzi mzuri sana.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved