Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, April 11, 2006
UTENZI WA AZIMIO LA DODOMA
Rabuka ulo enzini
Pumzi unijazeni
Niweze dondoa ghani
Malenga weza somani.

Mafuta tumepakwani
Tu safi twapendezani
Awali tulichekwani
Kwa kuto njia onani

Msaki kaambiwani
Dodoma njia fungani
Kafika kambaini
Miruko akichekani.

Keshoye wakaketini
Kazonta kimuitani
Na Martha kitokezani
Azimio liwekani

Kichaguana ngazini
Na katibu mpatani
Mawazo kiandikani
Kisha umma tangazia

Keshoye tukasomani
Na wito tutatoani
Azimio pokeani
Dira yetu angazani

Leo tunajigambani
Azimio kushikani
Wageni twawambiani
Jumuiya yaundwani

Niishe hapa sakini
Nipumue Kasirini
Gazeti Tando achani
Jina wazi tangazani.

Nimalize kwa thamani
Mkwinda kumuombani
Azimio lishikani
Na shairi litungani.
 
© boniphace Tarehe 4/11/2006 10:03:00 AM | Permalink |


Comments: 19


  • Tarehe 4/12/2006 4:45 AM, Mtoa Maoni: Blogger mzee wa mshitu

    Mkaruka

    Hili shairi lilifaa kupata tuzo katika mashindano ya kulienzi azimio la Dodoma maana vina vyake tu mi vyaniacha hoi vinavyomalizikia. Kwanini usitafute kaukumbi ndani ya hili kasri lako ambako katakuwa kanajaa haya mashairi tu maana nakumbuka unayo mengi.

     
  • Tarehe 4/12/2006 5:22 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    Hii ni fani. nakupongeza kwa jinsi unavyozidi kulifagilia azimio la Dodoma. tunasubiri lile la ughaibuni, ili tuweke pamoja na kubaini nini cha kuchukua kama ndio tamko la wanablog za kiswahili.

     
  • Tarehe 4/12/2006 8:01 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Haya haya bila haya,naanza kuingiliya,
    Makene ameingiya,Azimio kuungiya,
    Kanitaka kuchangiya,kwa tungo kuzitumiya,
    Pasi shaka nawambiya, kalamu nitashikiya,
    Ila kwa mukhtasariya, Azimio naungiya,
    Wa Dodoma wameonesha njiya, fikra zilotimiliya,Hima Miruko, Martha na wengine Azimio imarishiya.

     
  • Tarehe 4/12/2006 10:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Ushairi mnono sana huu.Cha muhimu ni kwamba azimio la Dodoma ni la aina yake na sote hatuna budi kuliunga mkono.

     
  • Tarehe 4/12/2006 10:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Ushairi mnono sana huu.Cha muhimu ni kwamba azimio la Dodoma ni la aina yake na sote hatuna budi kuliunga mkono.

     
  • Tarehe 4/12/2006 10:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Ushairi mnono sana huu.Cha muhimu ni kwamba azimio la Dodoma ni la aina yake na sote hatuna budi kuliunga mkono.

     
  • Tarehe 4/12/2006 10:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Ushairi mnono sana huu.Cha muhimu ni kwamba azimio la Dodoma ni la aina yake na sote hatuna budi kuliunga mkono.

     
  • Tarehe 4/12/2006 12:04 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Jeff naona umekuja na staili yako ya ushairi(hapo juu). Makene staili hii ya Jeff ni ile ya kisasa au ile ya kizamani (niipendayo mimi)ya vina na mizani sawa.(natania)

     
  • Tarehe 4/12/2006 1:04 PM, Mtoa Maoni: Blogger Mija Shija Sayi

    Mwaipopo unajivunja mbavu jamani..!!...hii staili ya jeff kweli ni ya aina yake.

     
  • Tarehe 4/12/2006 5:56 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Nani mwingine ambaye angekaribisha Azimio kwa ushairi kama si malenga wetu bloguni, Kasri mwenyewe? Sasa tunatazama kule kwa malenga wengine, nao watalikaribisha?

     
  • Tarehe 4/12/2006 10:34 PM, Mtoa Maoni: Blogger mzee wa mshitu

    Aaaah Mkwinda

    Nawe umekuja na yako mpya mizani yako nayo kama ile ya nani sijui pamoja na vina. Huraaah haya yote ni mambo juu ya mambo ukichanganya na shairi la Jeff lililo katika sijui chorus au vipi. Azimio la Dodoma+ ughaibuni+ Dar es Salaam+Mbeya+.... = mambo mazito ya blogu za kiswahili

     
  • Tarehe 4/13/2006 4:36 AM, Mtoa Maoni: Blogger ARUPA

    kwakweli mimi mashairi ya mkwinda huwa siyafahamu kabisa sijui ndio ushamba wa vina? huwa nahisi kama anachanganya na ki -mgonile!

     
  • Tarehe 4/13/2006 4:36 AM, Mtoa Maoni: Blogger ARUPA

    kwakweli mimi mashairi ya mkwinda huwa siyafahamu kabisa sijui ndio ushamba wa vina? huwa nahisi kama anachanganya na ki -mgonile!

     
  • Tarehe 4/13/2006 5:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger Christian Bwaya

    ama kweli bloguni kuna vipaji lukuki. Makene unatisha sana.

    Juzi nilishindwa kuungana na wewe on line. Kompyuta iligoma. Nilitamani sana ila ndio hivyo tena.

     
  • Tarehe 4/13/2006 8:43 AM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    afanaaalaeikh! yakhe waghani 'tafkiri watoka bumbwini! unatisha yakhe! kaza buti, haya mambo matamu ati...

     
  • Tarehe 4/16/2006 7:07 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Pandeni uwanjani kwangu muone nilivyoflow Kanzonta ananichengua anasema mie nachanganya na ki ugonile gonile teh teh yaani jamani utani kwenye blog unaleta rahaaaaaa hata kama mtu kakuudhi ukiingia Cafe'unaanza kucheka mwenyewe hadi watu wanakushangaa ngoja niwaonjeshe yaliyomo katika kibaraza cha FASIHI ZA UFASAHA:

    La Dodoma azimio, Makene limetulia,
    Lafaa kuwa zingatio,Bloguni kutumia,
    Tena liwe karipio, watakao vurugia,
    Azimio la Dodoma,liwe la wanaBlogu.

    Kwa uhuru twandikia, wengi wanatusomea,
    Maadili kupindia, hako wa kutukemea,
    Uhuru tunotumia, sote twaushere’kea,
    Azimio la Dodoma,liwe la wanaBlogu.

    Ni vijimambo tu panda huko uone utamu ulivyoanza kuvinjari ikwa vina na mizani sawia

    Wakatabahu

     
  • Tarehe 4/17/2006 5:29 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Waheshimiwa,hapo juu nilikuwa siandiki ushairi bali nilikuwa nagonga meza kwa kutumia mikono na sakafu kutumia miguu katika kuunga mkono hoja..

     
  • Tarehe 4/18/2006 8:55 AM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    malenga wetu makene, kaza buti
    kaza buti,

    wanenao na wanene, lakini hawakupati,

    we wa kwanza si wanne, katika mahanjumati

    taja pata na mapene, moyo ukikarabati

    hivo malenga makene, kaza buti kaza buti


    hahahaaaaaa. kumbe sijasahau. ebwana makene na mkwinda asanteni kwa kutekenya mistari yetu fofo...

     
  • Tarehe 4/22/2006 6:21 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Du kumbe Ustaadhi Michuzi wa Muhidini,yumo katika fani?

    Bali aikimbia fani, kwa kuogopa tufani,

    Upande wangu nadhani,Michuzi shika sukani,

    Bure waiona soni, shairi kuweka bloguni,
    Karibu katika fani, tenzi, shairi kuweka ndani.

    Wakatabahu

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved