Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, April 24, 2006
TAKRIMA YAENDA NA MKAPA!
MAHAKAMA kuu ya Tanzaniasijui ilikuwa imelala wapi miaka yote hiyo au ni kuonyesha namna mahakama zisivyo na uwezo wa kimaamuzi hadi pale zitakiwapo kufanya hivyo na serikali zilizopo madarakani, kama sivyo fikiri vingine lakini Tanzania ilibakia nchi pekee iliyokuwa imehidhinisha rushwa kuwa haki ya raia na kuiweka katika vitabu vya sheria. Sasa leo kama hujasoma hapa ni wakati wako pitia hapa. Ehee napumua, je vipi kuhusu kesi kwa wabunge na wagombea wengine waliotumia rushwa hiyo? Tuanze kufungua majalada sasa mahakamani?
 
© boniphace Tarehe 4/24/2006 04:45:00 PM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved