Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, April 19, 2006
SASA NI MIDRAJI IBRAHIM, MTEMBELEE BASI UONE
MWANANCHI, kunani pale, nikisema sana mtasema Kasri KUFAGILIA kumezidi. Hapana nadhani kama kuna tuzo ya kampuni inayohamasisha kumiliki Magazeti Tando kwa waandishi wake Tanzania ni Mwananchi. Siwataji leo waliokwisha kufungua makasri yao lakini leo hii ameingia huyu hapa muone wewe unayedhani huko Bukoba wamekaa wasiojua kompyuta.
 
© boniphace Tarehe 4/19/2006 01:20:00 PM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 4/20/2006 2:14 AM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Makene

  Huyu jamaa sina shaka atatupatia data za kina kuhusu kushindwa kwa 'babake' John Samwel Malechela, na za undani zaidi za wanasiasa na wengine wengi na hasa kwa kuwa tunafahamu pia naye ni 'Mwanamtandao'.
  Thidhani kama atatuangusha tunazisubiri data hizo hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi wa vigogo wa CCM utakaofanyika mwakani.

   
 • Tarehe 4/20/2006 11:30 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Makene, asante kwa habari njema hizi. Barua yako ya mama imenifanya nikusanye habari fulani njema kwa watu kama wewe ambazo nitazitundika bloguni. Kaza uzi...Mwananchi kule hakuna utani!

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved