MWANANCHI kumewaka moto, kila mwandishi anatakiwa kumiliki Gazeti Tando kabla mtandao wa Magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo haujakamilika na kuwekwa katika intenet. Absalom Kibanda mmoja wa wachambuzi wa juu kabisa wa masuala ya kisiasa katika Tanzania, mwenye uzoefu wa fani ya uandishi kwa miaka mingi naye ameitikia wito wa kufungua gazeti tando lake lisome hapa.
Halafu kama umempitia Msangi Mdogo utakuta kuna mapinduzi haya ambayo ameyaleta MK wa vijimambo. Wakati huo huo nashawishika kuamini kuwa anayetengeza mitandao ya blog za Tanzania anazidiwa kete kwa kuwa kama unatazama Athuman kapotea mtandaoni bila taarifa za kiufundi kutolewa.
Lakini haijatosha kuna mtanzania halisia ameingia pia mtembelee hapa. Huyu na mwingine sijui nani! Hapana nataka kumsalimu Mark Msaki na ndugu yangu Miruko kwa kubadili nyumba yake. Mapinduzi haya yananipa swali la kuhoji ni wapi mnapata mali hizi nyingi za kujenga mahekalu mtandaoni huku mimi ka kasri kangu kakibaki vile vile. Tunahitaji kuchunguza jitihada hizi za MK na kumpongeza maana sasa Magazeti Tando yetu yanapokelewa na kutanuka kwa kasi ajabu. Hureeeee asiye na mwana alale sisi Mwananchi tunazidi kupumua tuu. Wenye wivu ajinyonge! Charahani tunashukuru sana jitihada zako.
gazeti tando ndo nini vile?