Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, April 02, 2006
NINI TUJIFUNZACHO HAPA?
KAMA kuna kitu kilinipa mwaswali mengi kuliko majibu ni jeneza hili. Ilikuwa ni siku chache kabla ya kifo cha kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali ya Tanzania tangu uhuru. Sijui kama macho yangu hayaoni vema, lakini huu ni msaplasi unalimwa sana Njombe pale na unapatikana sehemu kadha Tanzania. Viongozi wa dunia hii ni maarufu kwa kuchongewa majeneza yenye kubeba gharama zinazoweza kusomesha watu elfu au kuchangia huduma za wananchi wao. Kikubwa hubaki swali la heshima hizo na matendo yao baada ya kupata nafasi ya kutumikia umma je huwa vinaambatana au kukaribiana au kuwa sawa? Je nini nafasi ya jamii hata mtu afarikipo? Tazama picha hii hapa.

 
© boniphace Tarehe 4/02/2006 04:11:00 PM | Permalink |


Comments: 9


 • Tarehe 4/03/2006 8:41 AM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Kaka hili tukio nalikumbuka na nilikuwa nikilifuatilia kwa karibu sana. Huu ni M-cyprus hakuna ubishi. Ubao huu ni wa bei ya chini sana, ubao usiokuwa na thamani, pengine kwa wenye mitizamo ya ajabu ajabu ya kupenda utajiri wanau-assume kama ni mti usiokuwa na hadhi ya kiongozi huyo.

  Hapa Tanzania hili ni ndoto watu wanazikwa siku hizi na masanduku ya plastiki, mengine ya chuma, mengine ya bati na mengine ya dhahabu wanatamani kuweka hata taa. Nadhani ingewezekana wengine wangewahifadhi wafu wao ndani.

  Lakini naambiwa pia kuwa hii ilikuwa zuga sababu ndani huyo dingi aliwekewa vipande vya thamani.

  Ciao

   
 • Tarehe 4/03/2006 10:50 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Hiki ni kitendawili Makene,jamii na ubinadamu huwa ni vitu vyenye kuchanganya sana fikra.Hivi nikifa hivi leo nitazikwa katika nini?Nafsi.

   
 • Tarehe 4/03/2006 11:11 AM, Mtoa Maoni: Blogger Michuzi

  makene umenikumbusha kitu. una habari siku hizi majeneza hapa nyumbani hutengenezwa kabisa, tofauti na zamani ambapo huchongwa mtu afapo? basi siku hizi karibu na lango kuu la muhimbili kuna maduka takriban manane na makampuni matatu ya kushughulikia maiti (nasikia hata watu wa kulia wa kukodi wapo). swali ni je, utamaduni wa kuchonga jeneza kabisa sawa hapa kwetu bongo?

   
 • Tarehe 4/04/2006 3:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Michuzi

  Umesema kweli, lakini nasikia nafasi zote pale Kinondoni zimekwisha kabisa kwasababu watu wameshanunua wakijitayarisha na maziko yao wakati wowote yatakapotokea. Ole wetu watoto wa walala hoi wa nchi hii mambo yameshakuwa mambo na sasa kila kitu ni business.

   
 • Tarehe 4/04/2006 6:54 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Kule Ghana kuna utamaduni wa kutengeneza majeneza ambayo yana sura ya vitu kama samaki, gari (kama Benzi), n.k! Utamaduni huu umepata umaarufu sana. Kuhusu kuchonga jeneza kabla ya kufa, watu wengi huwa na hofu kuwa ukichonga jeneza kabisa basi unakaribisha kifo. Ni sawa na hofu ya kuandika masuala ya mirathi, watu huwa hawapendi kuandika mirathi kwa hofu kuwa watakufa! Wakati mwingine kufa bila mirathi huleta ugomvi mkubwa kwenye familia.

   
 • Tarehe 4/04/2006 1:43 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Biashara ya majeneza ni poa kiasi. mambo ya maendeleo tu. Juzi hatukuwa na TV leo tunayo. Kuna dokta mmoja wa kutoka Ghana anataraji akistaafu kufundisha Marekani arejee Ghana kuanzisha biashara ya Mochwari. Hebu fikiria uswahili unaoukuta Muhimbili au hospitali ya Rufaa kule Mbeya. Maiti wako na rushwa unabidu utoe wewe ili nduguyo 'apendelewe' katika matunzo ya muda hapo. Azawaiz,...?

  Sasa biashara ya uhifadhi miili ya wafu haichukui nafasi inayostahiki hapa. Vile vile fikiria kijijini au mtaani kuna seremala wa majeneza mmoja halafu watu watano kwa mpigo wametangulia kunako jicho la haki siku moja. Si mtamtaka ubaya huyu bwana. Haichukui nafasi stahiki biashara ya majeneza hapa?

  Hakika lakini kama alivyosema Ndesanjo hapo juu inatisha na inasikitisha hivi. Lakini ni hali halisi.

  Kamtazamo tu.

   
 • Tarehe 4/05/2006 4:42 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

  Kufa siogopi, lakini sipendi kuendekeza fikra zinazotisha

   
 • Tarehe 4/05/2006 6:28 AM, Mtoa Maoni: Blogger Bwaya

  Wayahudi wao wanajiandalia makaburi yao mapema mapema wanachonga mwamba ili kuwapunguzia kazi waungwana.
  Kufa tutakufa iwe isiwe. Uandike mirathi usiandike, kuwe na jeneza au vinginevyo...kwa udongo tutarudi!
  lakini hata hivyo nani asiyeogopa kifo? Kama tungekuwa na uwezo wa kujua lini tutasitisha uraia katika tufe ya Dunia, sipati picha ingekuwaje. Ingekuwa ishu. Afadhali mambo haya yako hivyo yalivyo.

   
 • Tarehe 4/05/2006 6:43 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

  Kwa nini Makene umezua habari za kufa?

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved