Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, April 20, 2006
NI MAOMBOLEZO KWA WATANZANIA, HOUSTON TEXAS
HABARI hii nilitakiwa kuiweka hapa mapema kabisa lakini nashukuru kuwa imeweza kuwafikia wengi hata nyumbani kupitia mitandao mbalimbali. Ni kweli wenzetu wamepotea katika siku ya Pasaka, nilichokuwa nasubiri ni kupata picha zao ambazo waweza kuzitazama kupitia mtandao wa Watanzania wa Dallas Houston hapa. Kifo ni haki ya msingi kuliko haki nyingine kwa kila binadamu baada ya kupata haki ya kwanza yaani kuzaliwa na kuwa hai. Nitumie kauli ya mfalme Daudi ambayo nadhani itakuwa neno langu kwa wote wanaosikitika katika msiba huu. Ni kauli hii inayonifariji mimi na kunipa matamanio ya maisha ya ushindi anayoyajua yeye aliyenileta. "Bwana mimi ni nani na nyumba yangu ni nini hata umenileta hata hapa"

BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU!
 
© boniphace Tarehe 4/20/2006 11:11:00 AM | Permalink |


Comments: 3


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved