Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, April 06, 2006
NAVUTA PUMZI eeeeh!
KAMA kuna siku navuta pumzi ni leo, nina furaha sana hapa. Nini hasa nadhani wasema, Kasri kaanza hadithi zake. Lakini hapana nilikutana na Mmiliki wa Gazeti Tando la Kiingereza aitwaye Kabendera wa pale the Citizen Tanzania. Raha zaidi ni pale alipobainisha hili. Lione mwenyewe kwa macho yako. Je halikufariji, litakuwa wazi kabisa mwishoni mwa mwezi huu. Mambo saaafi.
 
© boniphace Tarehe 4/06/2006 11:23:00 AM | Permalink |


Comments: 7


  • Tarehe 4/06/2006 12:49 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Hii ndio maneno mi nataka.

     
  • Tarehe 4/07/2006 12:37 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    hata mimi nimelifurahia sana, baada ya kuliona kwa Ndesanjo. Mambo yazidi kupanuka, ingawa nahisi linaweza kuchelewa kidogo, kwani nimeona nafasi ya webdesigner imetangazwa upya kwenye mwananchi.

     
  • Tarehe 4/07/2006 5:02 AM, Mtoa Maoni: Blogger Innocent Kasyate

    Haya yatakuwa mapinduzi kwani bado magazeti yetu hayajapiga hatua kabisa katika hii mawasiliano ya umeme.

     
  • Tarehe 4/07/2006 5:10 AM, Mtoa Maoni: Blogger mzee wa mshitu

    Huree haya ndiyo mambo tunataka maana huku washikaji tupo katika kampeni ya kuhakikisha kila aliye Mwananchi anakuwa na ka-gazeti tando kake, msiwe na shaka wapo wengi wanakuja muda si mrefu watarajieni kina Abdallah Bawazir, Midraj Ibrahim na wengineo kama hao.

    Kabendera karibu bwana katika huu ulimwengu wetu wa kuchota fikra na kubadilishana mtandaoni hakika kuna chakula cha kutosha cha fikira.

    Ciao

     
  • Tarehe 4/07/2006 6:52 AM, Mtoa Maoni: Blogger Edison Ludovick Ndyemalila

    Na mimi kwa hilo nimwmkubali

     
  • Tarehe 4/07/2006 9:39 AM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    karibuni wote. kibanda na kampuni yako karibuni. sie wengine karibu tutaitwa wakongwe, kama si waandamizi, ila mtembeleeni ndesanjo kwenye tujikomboe tupate uhakika na uhalali wa neno 'gazeti-tando' ambalo mjadala wake unaendelea, na sifa zimwendee makene kwa kampeni yake ya kufanya kukubalika kwa jina hilo.

     
  • Tarehe 4/11/2006 3:27 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Makene mjanja sana anataka kujiweka katika historia,maana kafanya kampeni weee hadi kafanikiwa sasa gazeti tando hilooo latambulika laja kwa kasi kila mtu alijua, basi na kubaliane Blogu iitwe Gazeti Tando lakini tupige kura kwanza nani anakubali na nani anapinga ili uwepo uswa kwa wale waliotoa mawazo tofauti juu ya neno mbadala la Blogu

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved