Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, April 30, 2006
MKATABA KABLA YA KUJAMIIANA
BARAGUMU ana visa sana, siku zilizopita alinitumia E mail ikiwa na mkataba fulani nami nikauweka kando. Lakini leo nimetulia hapa na kuona umuhimu wa kupatia tafsiri ya Kiswahili ili uweze kusomwa na wanaume na wanawake wote. Mkataba huu umekuja baada ya kuongezeka matukio ya kesi za kubambikiziana kuhusu ubakaji. Usome mkataba huu hapa na ikibidi chapisha karatasi kadhaa za kutembea nazo.
 
© boniphace Tarehe 4/30/2006 01:03:00 PM | Permalink |


Comments: 8


 • Tarehe 5/01/2006 11:20 AM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Hongera kwa kulipamba kasri lako lakini hiyo saa uliyoiweka hapo juu kulia hatujui ni ya wapi Moshi au Ottawa au New Jersey.

   
 • Tarehe 5/01/2006 4:50 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Kasri linapendeza sana.Kwa bahati mbaya naona hizi rangi..nyeusi na nyeupe zinanipa tabu kidogo kusoma.Unaonaje?

   
 • Tarehe 5/01/2006 10:39 PM, Mtoa Maoni: Blogger Mija Shija Sayi

  Nilidhani nimepotea njia!

   
 • Tarehe 5/01/2006 11:40 PM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Hongera kwa kulipamba kasri lako , hivi mwenzetu tueleze hizi fedha za kujenga kasri kubwa kama hili umezitoa wapi tuelezea nasi, enhee sasa mbona hatuoni tena picha zetu tunapochangia, halafu chini ya makala zako mbona kiingereza bado hakijaondoka.

   
 • Tarehe 5/02/2006 3:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger tamba

  Yaani huu mkataba umenichekesha sana. Mkataba huo ni ngumu sana kusainiwa, mwanamke anapata wasiwasi, huyu mtu ananipa huu mkataba ana maana gani? yaani kwa kifupi unatisha. Halafu si unajua mambo ya ngono mara nyingine mnakutana kwenye pombe, na pombe ikiwa kichwani hata condom mtu unasahau achilia mbali mkataba! Ni mzuri lakini kwa huku bongo mgumu, sijui ughaibuni!

   
 • Tarehe 5/03/2006 12:32 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reginald S. Miruko

  Kweli hili kasri sasa linatisha kwa kila kitu, yaliyomo na sura yake. na pia kwa kazi ya kutafsiri mkataba wa kujamiiana, mimi ulinipitia nikaupeleka kwa wajumbe wengine kama ulivyo.

   
 • Tarehe 5/03/2006 12:35 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reginald S. Miruko

  MK naona sasa ni John Magufuli aliyekuwa anajenga nyumba na kuuza, kujenga na kuuza, kujenga na kuuza, lakini tofauti yake ni kwamba MK anajenga anagwa bure, anajenga anagawa bure hadi kila mtu awe na nyumba nzuri.

   
 • Tarehe 5/03/2006 11:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Makene,
  Nyumba mpya hii je kihamba ulikipata kihalali?
  Aisee, hongera kwa nyumba mpya. Picha na maneno pale juu naona rangi zake hazishabihiani vizuri.

  Mbele kwa mbele mkuu!

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved