Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, April 28, 2006
MAGAZETI TANDO MAWILI KWA MPIGO TENA
KAMA ulidhani MWANANCHI wanatania, umekosea kabisa. Kazi ya Balozi wetu mpendwa Mzee wa Mshitu, Yahya Charahani inazaa matunda sana. Tunatembea sasa kifua mbele tukiwakaribisha Angetile Osiah na Hawra Shamte! Wewe unadhani watu wadogo hawa, unafikiri wamekuja kujaribu, bonyeza yalipo majina yao kisha tazama kazi zao na kuwasalimia huko.
 
© boniphace Tarehe 4/28/2006 08:06:00 AM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 4/30/2006 12:53 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Ahsante Makene kwa kutuletea watu hawa.Nimewatembelea na kuwakaribisha.Mapinduzi yetu yanategemea watu,ni mapinduzi sawa kabisa na yale ya kina Chegu na Castro..watu ndio mhimili wetu.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved