Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, April 24, 2006
IPTL, ANGLO LEASING YA TANZANIA ISIYOTAMKWA
GAZETI Tando la Pambazuko limebandika ripoti inayotakiwa kusomwa na kila anayeitazama kwa jicho la mapendo Tanzania. Bado naipitia lakini nimeona nami niitundike hapa kama ambavyo wamiliki wa magazeto Tando mengine watafanya. Ina majina mengi tu yawe yametajwa kwa usafi au kwa uchafu lakini ina majina makubwa na linakosa jina la Rais wa Kwanza wa Tanzania tu, ambaye anaonekana kupaza kelele za kupinga hili dude liitwalo IPTL. Marais wengine wanaofuata wametajwa katika ripoti hii ikiwa ni pamoja na marehemu Horace Kolimba na wengine akina Rutabanzimba na Rugemarira. Isome hapa ripoti hii hapa na mjadala hautaisha sasa.

Katika tukio lingine, leo hii muswada wa BARUA KWA MAMA umekamilika ukiwa umekarabatiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa wanaweza kunisaidia kuusoma na kuuhakiki naomba msaada wao nami nitawatumia. Zaidi ya hapo ni malengo ya Kasri kuwa kitakapochapishwa kitabu hiki kitakuwa na kurasa za Magazeti Tando ya Kiswahili ili kutanua utangazaji wake.
 
© boniphace Tarehe 4/24/2006 04:29:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 4/27/2006 2:20 AM, Mtoa Maoni: Blogger Absalom Kibanda

    Nimeisoma hiyo Ripoti ya IPTL kwa umakini. Kwanza kabla ya kuingia katika mjadala naomba udfanye masahihisho yafuatayo katika majina ya hawa jamaa Rutabanzimba jina lake sahihi ni Rutabanzibwa na Rugemalira siyo Rugemarira.

    Ni bahati tu kwamba mwaka 1997-98 niliwahi kuandika habari kuhusu sehemu ya undani wa Mkataba wa IPTL, moja katika ya watu waliokuwa nikiwahoji akiwa huyo Rutabanzibwa, Mtanzania Mzalendo ambaye alifanya kila aliloweza kuupinga mkataba huo kwa malipo ya hata kutishwa.

    Kabla hajaingia madarakani, nilifanya mahojiano na Jakaya Kikwete kule Dodoma na moja ya maswali niliyomuuliza lilikuwa ni hilo la IPTL ambalo naye anaonekana kuguswa nalo na kukanusha kabisa kwamba aliwahi kuweka mkono wake katika jambo hilo.

    Hakika Watanzania bado tunapaswa kuuangalia mkataba huu na kuanzisha upya mjadala wa kitaifa kuhusu suala hili na kupambana hadi Wazalendo wa aina ya akina Rutabanzibwa washinde. Aluta Continua.

     
  • Tarehe 4/28/2006 9:58 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Kibanda endeleza mapambano. Mnaonaje habari yote hiyo ikatafsiriwa halafu itolewe kwenye magazeti ya kiswahili?

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved