Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, April 10, 2006
BARUA YA MAMA SEHEMU YA 6
KWA wasomaji wapya, KASRI anamuandikia mamaye barua baada ya kuhisi kuwa naye mbali. Katika barua hii anamkumbusha kuhusu matukio yanayotokea hasa Tanzania na kulinganisha na jamii iliyopo sasa. Leo hii anazunguzia kero za Wauza Baa maarufu kama " Bar maids." Soma uone nafasi yako kutokomeza unyanyasaji katika jamii yetu. Je na wewe unashiriki katika unyanyasaji huu, fuatilia kisa hiki kwa umakini hapa.
 
© boniphace Tarehe 4/10/2006 09:16:00 AM | Permalink |


Comments: 4


 • Tarehe 4/11/2006 5:38 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

  Makene naona una machungu, akisha yasoma yote haya, mama ataweza kustahimili ukweli huu?
  Na kama tutamtaka huyo mama awe na heri na maisha marefu si itakubidi ufiche ukweli huu?
  Lipi rahisi?
  Kazi safi, tena inaamsha hisia.

   
 • Tarehe 4/11/2006 7:18 AM, Mtoa Maoni: Blogger Bwaya

  Makene,
  Nashukuru sana kwamba teknolojia hii inaweza kutupatia mambo makubwa namna hii. Nimekuwa nikiifuatilia tangu ilipoanza ingawa sikuacha maoni. Kimsingi nina mengi sana ya kusema kuhusu Barua hii nzito ambayo imeibua mijadala isiyorasmi miongoni mwa vijana wenzangu.

  Naomba kujua iwapo naweza kuichapa na kuifikisha kwa watanzania wenzako hapa nyumbani ili mjadala uwe mzuri zaidi. Suala la haki miliki katika mtandao sina ujuzi nalo.

   
 • Tarehe 4/11/2006 9:16 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Mwandani shukrani, bora kunywea kikombe changu kuliko kukimbia mvinyo huu. Kikombe hiki nakishika lakini kigumu naona umeona hata wewe ila mapenzi ya baba aliyenituma yatime.

  Bwaya malengo ya Mgazeti Tando ni kufikishia taarifa umma mkubwa bila vizingiti. Ruksa wachapie na kuwafikishia maana imani yangu kuwa hakuna mtunzi atakayeweza kutunga haya maisha yangu. Ni mimi tu, maana asilimia kubwa ya barua hii ni ukweli na subiri mengi yanakuja.

  Makene

   
 • Tarehe 4/12/2006 4:53 AM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Makene

  Uchungu huu unaweza ukatufanya vijana tukashika mapanga na mashoka twende tukawakomboe mama na baba zetu waliopo kule Namagondo na kwingineko inatia uchungu inasikitisha. Tuhabarishe!

  Inawezekana miongoni mwetu tunaona ona tu halafu tunasahau, hatutilii maanani huenda mambo kama haya yakainua ari na nguvu mpya.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved