Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, April 13, 2006
BARUA KWA MAMA SEHEMU YA 8
BARUA imefika sehemu ya nane inayojadili maisha ya vyuo vikuu vya Tanzania na mfano chuo Kikuu Dar es Salaam. Nafasi ya serikali za wanafunzi namasaibu yake. Endelea kusoma sasa hapa sehemu hii ya nane.
 
© boniphace Tarehe 4/13/2006 09:07:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 4/14/2006 5:17 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

    Makene, Ijumaa kuu imenipa fursa ya kusoma nyaraka zako kwa kina. Sijasoma hii sehemu ya nane, nimeanza kusoma tangu sehemu ya kwanza kwa mara nyingine tena na ndio kwanza nimalize sehemu ya pili ya barua hii.

    Barua hii imenigusa, haswa sehemu ya pili unapomzungumzia mama kama mwalimu. na miye mama yangu alikuwa ni mwalimu, tena katika shule niliyosoma kama wewe, na mimi mama yangu alinichapa ili kuonyesha mfano kuwa hana upendeleo.

    Barua yako inanigusa roho kwa sababu nadhani japo ni ya kubuni ina ukweli mwingi sana ndani yake.

    Inanikumbusha kitabu cha mwanaharakati wa haki za watu weusi huko Marekani, George Jackson: The Soledad Brother.

    Kitabu hicho kilikuwa ni mkusanyo wa barua alizoziandika kwa familia yake na marafiki akiwa gerezani San Quentin. Kana kwamba ni za kubuni, barua hizo zilikuwa ni barua zenye mchomo mkali sana,
    Nakushauri ukisome kitabu hicho kama bado hujakisoma.

    Nakupa heko na hamasa: ENDELEA KUANDIKA. Kwani unawakilisha mawazo ya "Post indepenndence, post one party state Africa"
    Kama Ngugi alivyosema kwenye kitabu chake cha insha za: HOMECOMING

    "A writer responds, with his total personality, to a social environment which changes all the time. Being a kind of sensitive needle, he registers, with varying degrees of accuracy and success, the conflicts and tensions in his changing society. Thus the same writer will produce different types of work, sometimes contradictory in mood, sentiment, degree of optimism and even world view. For the writer himself lives in, and is shaped by, history."

    Naam, nimezisoma habari za kukanywa na mama yako - mama yangu pia bila ya shaka - Nimezisoma dhiki zilizowakabili waalimu wa wakati wa mama yako - mama yangu pia. Nimezisoma habari za TAMWA - African feminism. Nasema tena ENDELEA> Wakilisha kizazi chetu.

     
  • Tarehe 4/17/2006 2:40 AM, Mtoa Maoni: Blogger MICHUZI BLOG

    bonny, unaweza kuwa shakespear wetu kiutani utani tu. unajua hivi sasa hatuna tena kina kezilahabi, na hawa kina senkoro waliopo hawatoshi na wahitahika wengine wengi wapya? kaza buti kaka, fanya kweli... na hongera kwa kipaji cha kutisha

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved