MARK Msaki ametoka
Afrika Kusini na kufika
Dodoma kutekeleza jukumu la kupitisha Azimio la kutathimini taswira ya wamiliki na waandishi wa Magazeti Tando ya Kiswahili (Blogu). Safari hii ni ya pili kupata kuandikwa, ya kwanza ni ile Kasri alipoweza kukutana na
HARAKATI pale jijini Toronto. Kumekuwa sasa na mazungumzo ya wana magazeti Tando kila pande ya dunia. Jumuiya hii sasa inakuwa kwa kasi sana na hatukutarajia iwe hivi mapema. Kama mzazi unapoongeza mtoto ni jukumu lako kutafuta kitanda kipya. Kutokana na ukweli huu nasi tuna jukumu la kutafuta maadili yetu na tayari
AZIMIO LA DODOMA limepitishwa na hili chini ya Mwenyekiti
KURUNZI na katibu wake
MIRUKO na mjumbe mwenye heshima iliyotukuka
MARTHA na komredi
HUDSON KAZONTA. Kasri anapongeza na kulikubali
Azimio hili. Jitihada hii sasa inatupa picha kuwa baada ya siku si nyingi Magazeti Tando yatakuwa yakisomwa katika redio asubuhi na pia jumuiya yetu inaelekea kuzuri ambapo hata tuzo za mwaka zitafuatia hivi karibuni. Yote haya ili yafanikiwe yanahitaji wafanikishaji. Lazima kuwe na uongozi wetu wa kutuunganisha. Kamati ya Muda imepatikana na sioni sababu ya kuivua madaraka sasa hadi tutakapoamua vingine. Nikupongezeni na kukuombeeni pumzi ya mola muweze kutufikisha safari ya matarajio yetu. Asanteni, naomba kuwasilisha.
Asante sana kwa heshima uliyotupatia. wakati tunajadili na kutoa azimio la Dodoma, hakuna kati yetu aliyedhani tunafanya jambo kubwa namna hii. Nawashukuru kwa kulipokea na kulichapisha.