Ee bwana hii supu ilipikwa kwa saa nyingi kidogo kisha ikawa tamu sana. Lakini kapilipili kalikuwa kakali maana kalinitesa sana kuibugia. Enewei hii sijui niifananishe na supu ya wapi maana mimi Bongo si mtaalamu wa supu kama Fikra Thabiti ambaye alikuwa anatoroka shule kwenda kusaka thupu Kibororoni.
undefined
Hii maneno ya 'mtori' unafaa uwa-ge makini kuiandika hovyo maana watukumbusha mbali. Kiasili mie sio mla mtori. Nilipokuwa nauona ukitengnezwa na wenye asili nao kule Mbeya nikawa naunyanyapaa lakini siku nilipouonja mara ya kwanza pale Mlimani ndio nilipotambua kuwa ukitaka raha ya ngoma uingie na ucheze. Kunako mtori hunitoi hasa ile asubuhi ambayo jana yake 'ulizikamata' sawasawa (you know what I am saying, I bet so). Nafikiri Ndesanjo na Msaki wameshasahau hata unatengenezwaje.