Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, March 11, 2006
NINI MAANA YA MIKUKI HII KWENYE TOVUTI YA CHADEMA?

NIMEKUTANA na habari kadhaa baada ya kupitia tovuti za vyama vya siasa. Nitaandika makala haya baadaye. Leo kubwa ni hili na kipicha hiki kinachoelekeza wanaotaka kuwania ubunge na udiwani kupitia chadema, kuwa na kipicha hiki chenye mikuki miwili. Huko juu kuna habari kuwa hakuna kulala hadi kieleweke! Haya maneno si yangu waweza soma zaidi katika tovuti ya CHADEMA hapa na kisha kujibainishia ukweli mwenyewe.
 
© boniphace Tarehe 3/11/2006 11:27:00 AM | Permalink |


Comments: 8


 • Tarehe 3/12/2006 10:21 PM, Mtoa Maoni: Blogger Bwaya

  Ni muhimu kukumbuka kuwa CHADEMA kimekuwa kikitumia alama za kitaifa zinazotumika kuonyesha utaifa. Mfano nyuma ya picha ya aliyekuwa mgombea wa chama hicho, kulikuwa na bendera ya taifa. Helkopta iliyokuwa inatumika, ilipakwa rangi za bendera ya Taifa.

  Nadhani ndio maana wametumia alama hiyo unayoisema Bwana Kasri. Utakumbukuka katika nembo ya Taifa, kuna mkuki. Sikumbuki alama hiyo katika nembo ya Taifa ina maana gani. Ningejua basi ningefahamu kwa nini CHADEMA, chama cha siasa katiak Tanzania, kimetumia alama hiyo.

   
 • Tarehe 3/12/2006 11:22 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Bwaya umesema yoote. Nilipoisoma 'hii maneno' nilikuwa na kigugumizi kuchangia. Nilikumbwa na kigagasiko kwani sikujua kuwa pengine CHADEMA wanaashiria balaa. Kumbe yawezekana wanaashiria amani pale maadui wa Tanzania watakapopembejeka kuinyakua kwa namna yoyote iwayo. Nembo ya taifa haiyumkini inamaanisha hivyo. Pengine viongozi wetu watueleze vinginevyo. Hata hivyo nina shaka hawawezi kutueleza maana yoyote, mbaya au nzuri kwani hawana kumbukumbu vichwani mwao na vitabuni mwao. Si tunajua hawajui kama kulikuwa na hati ya muungano au la. Au kama ilikuwepo hawajui iliwekwa-ga wapi.

  Tukienda hatua ya pili tutajiuliza ile migolole (mashuka) na mikuki ambayo viongozi wetu aghalabu hupewa-ga (hata Kikwete alipewa-ga kule Arusha wakati wa kampeni) wakienda sehemu na sehemu inamaainisha nini? Inamaanisha amani maana amani ikiponyoka hairejeshwi kwa hotuba, si za Kiswahili wala kingereza, bali kwa ncha ya mkuki.

   
 • Tarehe 3/13/2006 8:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Makene,
  Nimeuona mkuki na pia kutembelea tena tovuti ya Chadema.Sikukawia kupata masikitiko kugundua kwamba chadema kupitia tovuti yao bado wapo kwenye kampeni na msiba wa mgombea mwenza.Hii ina maana vyama kama hivi huwa vinafufuka kipindi uchaguzi unapokaribia tu? Kimsingi kinaonekana kama hakina shughuli hivi sasa maana kama ingekuwepo basi ni muhimu sana kuweka habari zake kwenye tovuti yao.Karibuni habari zote zilizopo hapo kwenye tovuti yao ni zilipendwa.Hivi kinashindikana kitu gani?Chama kama Chadema kinashindwa vipi kuwa na webmaster wa kuipa uhai tovuti yao?Upinzani,upinzani....

   
 • Tarehe 3/16/2006 3:16 AM, Mtoa Maoni: Blogger msangimdogo

  Kwa kaulimbiu yao ya Hakuna kulala mpaka kieleweke, nina wasiwasi sana wasijewakajisahau na kusinzia maana itawachoma wao wenyewe, na hivyo walivyoisimamisha vibaya, sijui!!! Maana katika mazingira ya kawaida, tumeshazoeshwa kuwa siasa za Tanzania ni za uhasama na karibu kila linalozungumzwa huashiria shari dhidi ya fulani

   
 • Tarehe 3/17/2006 3:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Goda

  Nadhani inaweza kuwa ni kuponyesha majeraha ya kutumia fweza na hatimaye kuambulia patupu. wana hasira hawa jamaa. Hivi inakuwaje unatumia strateji zote na bado unabwagwa ka gunia vile? wakiamka mtaniambia.

   
 • Tarehe 3/17/2006 7:27 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Jeff: sio vyama vya siasa tu, hadi fani ya habari huwa ina magazeti yanayoanzishwa wakati wa uchaguzi na kufa baada ya uchaguzi. Tovuti hizi vya vyama nazitembelea sana. Unaweza, wakati mwingine, kupima umakini wa chama kwa kuangalia tovuti zao. Sasa mtunza tovuti yao sijui kalala? Wakati huo wanatuambia halali mtu...

   
 • Tarehe 3/18/2006 11:19 AM, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

  ni kweli na ninashangaa sana kwani kila nikizunguka utakuta angalau ni www.ccmtz.org wanaojitahidi tahidi kuupdate tovuti yao kwa habari mpya. ukienda www.cuftz.org au www.chadema.net yaani hakuna kitu. sijui wanashindwaje hata kutafuta vijana wa kuandika makala kama si kukusanya mawazo ya wanablogu na kuyatundika mtandaoni mwao......

  sio hivyo tu ila nimesikitia kusikia kuwa process ya kupata wagombea wa kuteuliwa nafasi maalumu imeleta mgogoro ndani ya CHADEMA........

  kinachoonekana hapa ni pamoja na kuwa suala la ruzuku bado linaleta mgogoro kwa vyama vilivyopigwa dafrau katika uchaguzi, bado suala la kuwa serious bado halijaoneka karika upinzani ndiuo maana wananchi huhofia kupoteza muda kuwaunga mkono!!

  kama wako serious, kwa nini wasiungane sasa hivi? wanasubiri mpaka 2010 wakose kiti hata kimoja? kuna dada mmoja hapa wa kikenya ambaye huwa hayuko katika siasa lakini akanihoji siku moja...hivi nyie mko sawa kweli? wagombea wote wa uraisi wanatafuta nini??

  suala la mkuki....naona tuwaulize wenyewe...labda wanamkumbusha CCM aende taratibu maana mkuki kwa nguruwe.....

  hivi Makene unablogu ngapi?

   
 • Tarehe 3/18/2006 12:53 PM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Nina Ndesanjo moja ambayo sijaweka kitu na hii hapa. Si unajua suala la kushika jina asije akaibuka mtu kwenye Word press huko akajiita KASRI LA MWANAZUO. Naomba Mola afanikishe fikra zangu Blogu hii iwe Gazeti kabisa la kusomeka Tanzania katika miaka michache ijayo.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved