Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, March 23, 2006
KUMEKUCHA, AMKA BLOGU NYINGINE TENA YAINGIA
HUYU jamaa ni moja ya watu ninaopaswa kuwashukuru kwa mengi. Msomaji wa makala zangu Tanzania anaponiandikia kushukuru kuhusu maandishi yangu kimsingi anakosea. Huyu jamaa ndiye chanzo cha nafasi hii, anapaswa kushukuliwa huyu kwanza. Sasa baada ya kimya kirefu ameamua kufungua Blogu yake isome hapa. Nasikia kuna mkakati kwa waandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication kufungua Blogu zao ikiwa ni mkakati wa awali kabla ya magazeti hayo kuwekwa mtandaoni hapo baadaye mwaka huu. Mtembelee Yahya Charahani na kumsalimu kama ilivyo ada yetu. Naona anajiita hivi...KARIBU YAHYA saaaaaafi sana.
 
© boniphace Tarehe 3/23/2006 06:59:00 AM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 3/24/2006 11:57 AM, Mtoa Maoni: Anonymous frankgeofray

    haya makene tumesha mtembelea na tumemkaribisha,sasa kwanini hujaweka blog yangu kwenye kipengele chako cha blog za wenzangu?ni www.fglukwaro.blogsport.com

     
  • Tarehe 3/25/2006 11:48 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

    Kweli Kasri, umesema sawa: kumekucha. Asante kwa kututaarifu.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved