Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, March 21, 2006
BLOGU NYINGINE HIYOOOOO
KABENDERA ni mwandishi wa Habari wa Gazeti la The Citizen la Tanzania. Amefungua ukurasa huu na kujiunga moja kwa moja na familia ya NDESANJO katika wordpress. Mtembeleeni, lakini sijui maana kizungu mimi kwangu kigumu kuandika sijui huyu jamaa atafanyaje ili aninase huko kutoa maoni mengi...enewei suala la kutanuka Blogu linatia moyo sasa hivi si kwamba tunashawishi watu kuingia ila wao wanafungua kabisa na kutoamba kuzitangaza. Miaka ijayo huduma ya kutangaza Blogu itakuwa inalipa...sijui Ndesanjo atatengeneza dola ngapi kwa huduma hii...yatatokea mtembelee KABENDERA na kunywa kahawa kwake hapa.
 
© boniphace Tarehe 3/21/2006 10:17:00 AM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 4/06/2006 5:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger Mwavizo

    Nakuona ndugu yangu kweli unasambaza habari kuhusu blog zetu sisi tuliopo nyumbani. Nimepitia blog yako na nimefurahishwa na baadhi ya mambo niliyoyasoma.

    Kusema kweli umenipa changa moto nami pia nitaanza kutuma habari mbali mbali kwa Kiswahili.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved