Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, March 26, 2006
BARUA YA MAMA SEHEMU YA 3
KASRI anafafanua masaibu yanayowakabili wastaafu wa Tanzania katika Barua hii ya aina yake. Endelea kupata nini kinaendelea na pita hapa mara kwa mara kupata muendelezo wa Barua hii ya Kasri la Mwanazuo kwa mama yake Esther Makene. Sasa endelea na sehemu ya tatu hapa. Usisite kutoa maoni kuhusu barua hii.
 
© boniphace Tarehe 3/26/2006 11:41:00 AM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 3/27/2006 1:20 PM, Mtoa Maoni: Anonymous mtandawazi

  Nikidhani mamake Kasri angali ameambukizwa ugonjwa na wanajamii. Hajui kwa nini mwanawe mwenye elimu na mwerevu angali maskini akilinganishwa na yule kijana mwenzake.

  Nia yake kumpa elimu kijana wake ilikuwa apate kazi atajirike siku za usoni. Hii ndiyo ndoto kizazi kinachopita kimelazimishwa kuota na viongozi wa bara la Afrika. Aghalabu utawasikia wakisema...

  " wapeni watoto elimu kwani mnawajengea msingi mzuri wa maisha.."

  Lakini ukweli unabakia kwamba kazi zinazolingana na elimu sampuli ya kijana Kasri zinapewa wana wa walio katika uongozi.

  Vile vile babake kasri hawezi kutambua sababu ya wastaafu kutollipwa marupurupu yao. Alidhani Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mahali pema pa kufanya kazi. Lakini haiwezekani iwapo viongozi wana mtazamo tofauti na wake Kasri.

   
 • Tarehe 3/30/2006 9:44 PM, Mtoa Maoni: Blogger charahani

  Makene huyu mamake Kasri ni amenikumbusha mbali sana sawa na mamake Mzee wa Mshitu akiwa kwao kule Namagondo, au Murutunguru, au wapi sijui kule Kisorya anatarajia maisha kuwa asali na maziwa baada ya eti kumpeleka mwana shule lakini anakuja kukatishwa tamaa mtoto ameelimika kazi hapati na hata akipata anapata kazi ya mshahara wa kijungu jiko kazi zote nzuri zinakwenda kiukoo.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved