Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, March 25, 2006
BARUA YA MAMA (2)
KASRI anaendelea kumuandikia mama yake Barua, Barua hii ni muwali kwa akina mama wote wa Afrika na inafaa kusomwa na akina Baba pia. Barua hii itakuwa ikiendelea hapa na kuhifadhiwa katika makala za Weledi wa Kasri La Mwanazuo. Lengo ni kuwa Riwaya hapo Baadaye:

Waweza kuendelea kusoma muendelezo wa Barua hii hapa kama umeshasoma sehemu ya kwanza hapo chini. Nakutakia usomaji mwema.
 
© boniphace Tarehe 3/25/2006 12:06:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 4/02/2006 9:38 AM, Mtoa Maoni: Blogger Mija Shija Sayi

    Makene kwanza nikusifu kwa barua yako kwa mama Esther ingawa mimi naitafsiri kama barua kwa mama yako TANZANIA.

    "Mama yetu TANZANIA amezaa watoto wengi wenye vipaji na uwezo mbalimbali, licha ya kuwa watoto hawa kuwa ni wengi mno lakini wana bahati ya kuwa na utajiri wa kila kitu kuanzia maji, ardhi yenye rutuba, watu wenye nguvu na afya bora, wanyama na hali ya hewa nzuri. Lakini maskini ya Mungu watoto hawa wameshindwa kabisaa kumudu utajiri huu, mwanzoni kidogo ilianza vizuri kwani kaka na dada zetu wakubwa walijitahidi kutufundisha kuishi kwa ujamaa mambo mengi yalienda vizuri, lakini baada ya hao kupita waliorithishwa wamekuwa ni taabu tupu, wengi wao wameingiwa na ubinafsi na kutuacha wadogo zao tukisota"

    Makene hiyo ni picha ambayo nimekuwa nikiipata katika barua yako kwa Mama. Kuna hili jambo la Tamwa ambalo umelitaja katika waraka huu wa pili, hivi ni kwa nini haya mashirika haya huwa hayaelekezi nguvu zake vijijini zaidi? Tamwa ni shirika lenye nguvu sana lakini sasa hivi ukiwauliza kina mama kutoka Kukirango, Nyamurandirira, Suguti n.k ..juu ya shirika hili hubaki wakikuangalia labda kidogo Butiama, ingependeza mashirika haya yakafungua matawi katika kila kata za mikoa ya Tanzania ili kupata taarifa nzuri na za kweli kuhusu jamii husika, huu mtindo wa kuchukua taarifa za jumla hauwezi kuleta mabadiliko, na hii ni kwa mashirika yote.
    Mama yetu Tanzania hafurahishwi na hali hii jamani.

     
  • Tarehe 4/02/2006 11:08 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Mija nashukuru sana, si unaona raha ya kuandikia kitabu mtandaoni. Yaani hapa umeniongezea wazo na sasa simuwazi zaidi mama Esther, Makene, sasa naingia kumuwaza Tanzania na huenda baadaye atakuwa Afrika. Nashukuru sana kwa mnaosoma na kuchangia mawazo yenu. Nayaheshimu sana na ninayapa tuzo kuu moyoni mwangu. Naamini hamtakataa kama nikifikia lengo la kukamilisha kazi hii ndipo niwaandike kwa majina wale nionao mchango wao umekuwa mdogo hapa na ninyti mliotoa mchango mkubwa nikawahifadhi moyoni. Kubwa jingine hivyo vijiji ulivyotaja, nambie umeishi huko? Isingekuwa rahisi mtu wa kuelezwa tu akavitaja kwa mfuatano bainifu kama huu. Mija kweli sikuwezi!

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved