Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, March 24, 2006
BARUA KWA MAMA 1
KASRI la Mwanazuo anaanza kutoa Riwaya yake ya Barua ya Mama, ikiwa ni mkakati wa kuongeza machapisho ya Kiswahili. Riwaya hii anamuandikia Mama yake Esther Makene ikiwakilisha migogoro na masaibu ya jamii ya Afrika na ikionyesha baadhi ya uzoefu wa Kasri katika nchi za Amerika. Karibu hapa usome sehemu ya kwanza.
 
© boniphace Tarehe 3/24/2006 11:09:00 AM | Permalink |


Comments: 5


  • Tarehe 3/24/2006 3:07 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    you are an Amaizing KID..
    you are BLESSED..yu are SPECIAL..
    Duu..machozi yananilengalenga!!

     
  • Tarehe 3/25/2006 2:23 AM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

    Hongera makene.Nimeelewa mengi katika barua hii kwa mama yako ambaye bila shaka anawakilisha wengi wetu.

     
  • Tarehe 3/26/2006 1:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

    Mozowe. Nianzie wapi kutafakari waraka huu. Nadhani ni waraka wa kubuni lakini ni dhahiri kuwa unafanana na kweli.
    Kitu kimoja kigumu kwa mwandishi yeyote ni kuongopea karatasi. Midhali umetwaa kalamu na kuanza kuandika basi hizo fikra, simanzi, maswali na majibu nayo yanapita kwa kasi akilini.
    Nimeburudika na kuwaza pia. Nakuzerwa - Mtanzania katika muhtasari.

     
  • Tarehe 3/28/2006 9:39 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Waraka uliojaa maisha..huu ni mtiririko mzuri sana wa maisha.Hayatakiwi kuwa hivyo.Kwa bahati mbaya wengine ndio wanaokabiliwa na hali hiyo huku wakidhani ni hali halisi.Ukombozi ndio ufunguo wa mbingu za duniani.Nafasi ya jamii,jamii ni mimi na wewe,kujionyesha na sura ya malaika.Salamu kwa mama.

     
  • Tarehe 3/29/2006 5:15 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Makene, nimekuwa nikisubiri sana utufaidishe kwa kipaji chako cha kuandika riwaya. Kuna jambo tuliongea siku moja, najua sijatimiza ahadi. Kisa hiki kimeniamsha. Nitakuandikia kukupa zile "kodi" za kutoa blogu ya kitabu. Mchanganyiko wa wanablogu wenye vipaji na ujuzi mbalimbali unafanya jumuiya yetu kuwa ni kijiji fulani. Na unajua tutaweza kujenga nchi kwa kuanza kujenga kijiji.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved