Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, February 12, 2006
WANASIASA BWANA, WE ACHA TU?

Pius Ng'wandu alitangaza kujiondoa katika siasa. Kama walivyo tabia yao kumbe ilikuwa ni danganya toto. Juzi juzi akajitutumua tena kutaka ubunge wa Afrika Mashariki na kudondoka katika hatua za chama. Hivi huwa hawakumbuki wanayotangaza au ndiyo siasa hiyo? Hapa akiwa na Mbunge Aziza mwenye Kitenge safi pembeni mwa Kasri, hiki ni kikao cha kujadili madhara ya Bodi ya Mikopo Tanzania iliyoambatana na mgomo chuo Kikuu Mlimani.
 
© boniphace Tarehe 2/12/2006 01:23:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 2/16/2006 1:57 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    duh mbunge Aziza bado ni muheshimiwa? nilikutana naye uwanja wa ndege mwanza 2004 february...wakati nikwa ninaunganisha ya kwenda bukoba naye alikuwa anakonect alikuwa ana msiba nadhani!!msalimie sana!

     
  • Tarehe 2/23/2006 4:44 AM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

    Nakukumbuka sana makene ulivyokua mpashaji habari wetu hodari pindi utokapo wizarani.Mara nyingine mlikua mkienda kama mbogo na mnaporudi kimya kama mmemwagiwa maji.

    Ilifika mahali hata imani za wanafunzi ikaanza kutoweka kutokana na kauli za baadhi ya viongozi wenzako(wewe haumo).hapa sitachoka kumuongelea kihomoni!!!!!!!!

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved