Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, February 11, 2006
ULIMWENGU JIRANI NA KASRI

KWA wasiomfahamu Jenerari Ulimwengu nawapa pole. Ni huyu shujaa aliyekubali kuanika uwazi wa Mkapa kupalilia rushwa nchini. Shujaa huyu amechapisha kitabu cha makala zake na mfano huu utaigwa na Kasri la Mwanazuo ambaye anapanga naye kuchapisha makala zake kuwa kitabu kitakachojulikana kama Weledi wa Kasri la Mwanazuo. Ulimwengu yu katikati na pembeni mwenye Koti jeusi ni Kasri, ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam.
 
© boniphace Tarehe 2/11/2006 11:49:00 AM | Permalink |


Comments: 4


  • Tarehe 2/11/2006 2:59 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Kumbe Ustaaadhi Jenerali naye anagida mango juice?

     
  • Tarehe 2/12/2006 6:35 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Kitabu cha Makala za Ulimwengu nimekisoma. Ulimwengu ni mmoja wa watu ambao si wavivu kutumia akili zao kabisa. Kitabu kinapatikana TPH kwa bei ya 5,000 tuu

     
  • Tarehe 2/12/2006 11:32 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Idya unafatilia sana mambo, kuna haja mawazo yetu tuyahifadhi pia katika vitabu ili yaweze kutumika kwa miaka na miaka.

     
  • Tarehe 2/15/2006 8:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    tunashukuru nikitua nitakitafuta.... tunamshukuru mungu pia amempa maisha hadi leo hii tutasoma vitabu vyake! Tanzania ya sasa inataka watu wanaopenda kutumia akili...

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved