Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, February 06, 2006
MSIMAMO WA KASRI KWA HOJA YA WABUNGE KUJINEEMESHA
NIMEPOKEA barua ya intanenti kutoka kwa jamaa aliyejiita jina la REKEBISHA TABIA. Kama lilivyo jina lake sikupata hofu ya kumfahamu nia yake. Niliposoma nikaona niwahabarishe wana KASRI ili nao waweze kujua kinachojili baada ya makala zangu nilizozirusha kupitia Gazeti la Mwananchi linalochapishwa nchini Tanzania. Soma eneo la barua ya Rekebisha Tabia kama nilivyoinukuu katika barua zangu za intaneti.
Nimesoma makala zenu mbali mbali na kuona nyie wanahabari mmeifungia kibwebwe sana hoja ya wabunge kuomba maslahi zaidi.
Ama kwa hakika mtu upewapo kazi ndipo unatakiwa uweke sawa hoja zako na hasa za maslahi.
Mimi kazi za ubunge sizijui uzito wake hivyo inaniwia vigumu kutathmini mshahara na marupu rupu yake lakini haya mashambulizi dhidi ya wabunge yakiongozwa nanyi wanahabari yananitia mashaka juu ya nia na dhamira yenu. Nina hakika kila mtu anayohaki ya kusikilizwa , hofu yangu nia hii hukumu iliyokaa ki wivu wivu, kikauzibe,nk....
Nashauri hoja zao zipewe uzito unaostahili na hasa kwa vile wameziletwa kiungwana na bila vitisho.
Aghalab pia utasikia watu wakisema vibaya juu ya 'mashangingi' wanayokopeshwa ili kuhudumia wapiga kura wao, kwa wivu tu.
Naomba mfikirie upya changamoto zenu.
 
© boniphace Tarehe 2/06/2006 08:03:00 AM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved