Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, February 06, 2006
MKAPA ALIPALILIA RUSHWA?
SIKUBALI kuamini kama ni majibizano yaliyotokana na Jenerari Ulimwengu kufutiwa uraia wa Tanzania katika kipindi cha serikali ya Mkapa, kuwa ndio chanzo cha kauli hii ya Ulimwengu aliyoitoa Tanzania siku chache zilizopita. Kwa kipindi kirefu KASRI limekuwa likiutazama uongozi wa serikali ya awamu ya tatu sawa na ufalme. Ilikuwa ni serikali iliyowanyima fursa wenyeji, kuwathamini wageni na kuwakweza matajiri. Ni serikali iliyotanua wigo mpana sana kati ya maskini na tajiri. Sula kubwa la rushwa lilitangazwa rasmi kuwa moja ya vivutio vya kuwekeza Tanzania na bunge likapitisha kula rushwa kuwa haki. Soma zaidi makala hii hapa.
 
© boniphace Tarehe 2/06/2006 08:52:00 AM | Permalink |


Comments: 8


 • Tarehe 2/06/2006 10:19 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

  Kuhusu swala la rushwa kumalizika nchini Bongo ndugu yangu Makene ni ndoto kwani mikono yawanaopiga kelele juu ya mapambano dhidi ya ufisadi huo imekithiri.Inasadikiwa ndiyo hao hao wanaong'ata na kupuliza.Ndiyo hao wanaopinga wala rushwa huku wakipokea na kutowa rushwa.

   
 • Tarehe 2/06/2006 12:09 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Nikishafanya 'kwiz' kesho nitakuwa nimekwisha kusanya ufahamu yakini kuhusu namna mlungula ulivyoshadidiwa katika awamu ya tatu ya utawala wa Bongo.

  Kwa sasa ntawapa mfano mdogo tu. Kuna mwalimu mwenzangu kule TIA Mbeya (zamani DSA) ambaye hukengeusha uneni "Rushwa ni adui wa haki" na kuuita "Rushwa ni rafiki wa haki".

  Hasemi tu hivihivi. Hapana. Mara zote hukazia hoja yake hii na jinsi Tanzania ilivyo kwa sasa. Huainisha upatikanaji wa huduma anuai kama vile umeme, maji, afya, polisi na kadhalika. Ukitaka kupata moja ya huduma hizo hapo kwa kufuata utaratibu husika itachukua mwaka moja ama miwili. Kama ni hospitalini si wewe ama ndugu yako atakuwa amekufa? Sasa unapotumia rushwa unapata umeme kwa siku mbili tu, maji siku hiyohiyo na kadhalika.

  Hoja yangu hapa ni kuwa rushwa ama ufisadi kama inavyoitwa kule Kenya imeoteshwa mizizi hata sasa inaonekana ni sahii kushiriki na ni haramu kuwa msafi. Yoote hii kwa sababu ya kufumba macho kwetu.

   
 • Tarehe 2/07/2006 2:15 AM, Mtoa Maoni: Blogger must

  Mkapa au Mr clean kama alivyojulikana na rafiki zake alikuwa safi kweli kweli. Wakati wa utawala wake alianzisha kikundi cha Maigizo alaliita PCB. Kikundi hiki kilifanya maonesho kwa kuigiza kowakamata walimu, mahakimu wa mahakama za mwanzo, makarani wa mahakama huku uhakisia wenyewe wa rushwa ukusifiwa kutungiwa sheria za kuulinda na kutoa maneno ya kejeli kwa waliokereka. Utaulizwa "wewe unaongelea rushwa na sisi tukikuuliza hilo shati la bei mbaya ililovaa umelipata wapi utajibu nini" ulimwengu aliulizwa alipotoa mtaji wa kuanzisha Habari corporation ati.

  Huyo ndio mr clean eti nasikia sasa amehodhi mashamba kule Lushoto na pia ni mwanahisa katika kiwanda cha miwa cha mtibwa pamoja na kuwa na mashamba ya kufa mtu aliyoyadhulumu kutoka kwa wakulima wanyonge wa kule.

  mr clean hakupendwa rushwa na ilimkera kweli kweli yeye alipenda vizawadi vidogo vidogo na takrima ooooh muda wa kukatiwa umeme umewadia kama ratiba inavyoonesha ah...

   
 • Tarehe 2/07/2006 8:40 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Makene,
  Nadhani kichwa cha habari yako ni kweli tupu.Mfano mdogo ambao ninautumia katika kutambua haya ni muundo wa tume lukuki ambazo ripoti zake hazikuwahi kuonekana na wala kusomwa na kufanyiwa kazi.Sasa hilo ni kumbato gani kama sio la rushwa???

   
 • Tarehe 2/09/2006 1:00 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

  Unajua kuna matatizo mengine hayahiyaji nadharia kushughulikia. Kama alivyosema mmojawetu hapo juu kilichofanywa na serikali ya Mkapa ni kuunda taasisi kibao ambazo ziliitwa za kupambana na rushwa. Wakaandika juzuu na majuzuu kuhusu nadharia ya rushwa na namna ya kuikabili. Wakapata fedha toka kwa wafadhili. Miaka kumu ikaisha kwa kuwa na majuzuu bila upambanaji wowote wa rushwa.

   
 • Tarehe 2/09/2006 1:53 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reginald S. Miruko

  Kauli ya Jenerali Ulimwengu haikumwagiwa petroli na kuporwa uraia, wala kurejeshewa kurejeshewa uraia kwa mbinde baada ya wapenda haki kulalamika.
  Ni kauli yake ya muda mrefu na kwa taarifa yako, ndiyo iliyochochea apokonywe uraia wake. Ukisoma kitabu chake Rai ya Ulimwengu' kilichokusanya makala zake zote alizotoa kwenye Gazeti la Rai miaka ya nyuma, utajua kuwa kichwa chake hakipendi ufisadi.
  Naamini ni kweli Serikali ya Mkapa iliendekeza Rushwa. Mkapa hakupenda kusikiliza malalamiko ya wananchi dhidi ya mteule wake yeyote. Ngoja tuone JK

   
 • Tarehe 2/09/2006 9:33 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Ni kweli Miruko naona umrenikumbusha jukumu la mimi pia kuchapisha makala zangu kuwa kitabu. Maana ni katika namna hii tunaweza kuweka kumbukumbu ya misimamo na imani zetu. Suala la Rushwa siku zote nimezungumzia nafasi ya Mfalme Mkapa katika kuitanua na hili halina uongo.

   
 • Tarehe 2/15/2006 7:59 AM, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

  Kasri, kuna wakati ilifika ikahojiwa kuwa PCB imekuwa ikitafuna hela bila output...labda sasa JK ataielekeza majukumu yake!

  juzi wamekamata polisi nadhani tunduru kala rushwa ya 10,000 / = eti mtu kampiga mwenzie, jamaa kenda shtaki, polisi katoka kenda kuriaresti rijamaa, walipofika polisi majamaa yakakubaliana yakamalize ishu nje, polisi akayadai chau chau naona cha usumbufu wakaenda kumletea ya moto!!!! ja ja hapo mnasemaje wandughu!! na imetangazwa kweli!!!

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved