Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, February 12, 2006
MAMA MIGIRO NAYE?

HAPA ni waziri wa Jinsia na Mbunge anayewakilisha jimbo la Vyuo Vikuu. Kuna kauli alinipa nilipomuuliza swali fulani...kama kweli anakumbuka sasa ajikaze maana aweza kuwania urais baada ya Kikwete.
 
© boniphace Tarehe 2/12/2006 01:27:00 PM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 2/13/2006 5:17 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Huyo jamaa aliyeko kulia alituchekesha sana siku moja. Nilikuwa katika kamati ya kuchuja wagombea wa uraisi, makamu wa raisi na kadhalika. Alipoingia katika kitimoto Albert Msando akamuuliza rangi ya soksi zake. Kumbe lilikuwa swali baya sana kwake kwani hakujiaandaa kwalo. Huku akitetemeka akavuta suruali yake juu na kusema kwa kweli jamani leo sikuvaa soksi kabisa. Kweli hakuvaa. Lakini kama umuonavyo mzee wa suti kweli-kweli. Katu huwezi kudhani huwa havai soksi. Nimemsahau jina ila nilikuwa nikimwita 'Jidulamabambasi'

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved