Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, February 09, 2006
MAHITA ANAPOGOMA KUNG'OKA?

MAHITA mkuu wa Polisi jeshi linashirikiana na majambazi huko Tanzania ametangaza hivi. Katika kipindi cha madaraka yake amewatia mauti watanzania lukuki kutoakana na vifo vya majambazi na polisi huku akiuacha umma katika misingi ya utengano na sasa anatangaza kuwagawa wananchi kwa misingi ya siasa. Yeye kwake madaraka ni muhimu kuliko kujua namna ya kuwajibika. Amenonewa na madaraka, hajui kuwa kazi ikukushinda unapumzika. Anasubiri kuondolewa kwa nguvu na kwa kauli zake dhidi ya CUF chama cha siasa mbadala Zanzibar zinaonyesha namna wazi alivyokuwa akilitumia jeshi hilo kuwadhibiti. Anaapa kuwa CUF hawatashinda kamwe akiwepo soma makala hii hapa.
 
© boniphace Tarehe 2/09/2006 01:12:00 PM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 2/12/2006 6:57 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Na wewe Mahita achia ngazi tu. Umekula vya kutosha na sasa waachie wenzako wajaribishe nao.Huoni hata hilo tumbo lako lilivyotanuka utafikiri unakaribia kujifunguwa?Au unaogopa utapatwa na unyafuzi wa fedha baada ya kutoka madarakani?

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved