Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, February 11, 2006
KUTOKA URAIS WA WALIMU HADI UWAZIRI WA ELIMU

KATIKATI ni mama Sitta waziri wa Elimu wa sasa siku ya Uzinduzi wa Chama cha Walimu Wanafunzi Chuo Kikuu Dar es Salaam. Kasri alikuwa Makamu Rais wa Kwanza wa chama hicho na hapo anaonekana akiwa na shati la njano.
 
© boniphace Tarehe 2/11/2006 11:46:00 AM | Permalink |


Comments: 8


  • Tarehe 2/11/2006 1:30 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Mmependeza wenyewe utafikiri mmemaliza kupata bumu la kikao.Halafu ndugu yangu Makene mbona poti wako ndiyo wengi kwenye picha hiyo?Au kwenye utawala wako undugunaizesheni uliutanguliza mbele?

     
  • Tarehe 2/11/2006 1:48 PM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Nitakutaja jina maana nakufahamu kabisa licha ya kujifanya anonimasi. Tazama hapo upoti uko wapi, hao wote ni walimu sasa ulitaka tukuchukue na wewe wakati hukuwa mwalimu? Ee bwana acha utani maana unajua kuwa uchaguzi wa UDSTA ulikuwa unafanyika kwa demokrasia kabisa na Rais wake wa kwanza alikuwa Kahangwa na huyo si poti wangu. AAH LAKINI UMENIKUMBUSHA UTANI WA SIKU NYINGI KAKA ANONIMASI AMA.....B....sujui.

     
  • Tarehe 2/11/2006 2:57 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Ingawaje sikuwa-ga mwanafunzi wa ualimu Mlimani lakini kampani yangu kubwa ilikuwa-ga wanafunzi wa Ualimu. Mbali na Kahangwa na Kasri namuona Nyamubwe Goodluck na Karuti Bugwema. Huyo muiraq (ya Arusha sio Baghdad) kulia kwako kajina kake nimekasahau ingawaje alikuwa-ga mshikaji wangu kwenye tu-siasa twa Mlimani. Hebu nikumbushe ka-jina kake. Waliosalia majina yao ya ki-Musoma magumu kuyakumbuka.

    Kuhusu suala hili la kaukabila mie pia nalipinga. Kilichokuwa kikitokea Mlimani ni kuwa hawa majamaa yalikuwa-ga na tabia ya kujitokeza kugombea-gombea katika kila nafasi inayojitokeza ya uongozi. Wengine tulikuwa tunawaangalia tu. Nakumbuka niliwahi kusimama nao katika gombezi (chaguzi) fulani. Ila inapokuja suala la sera ndio huwa-ga hawana-ga za kutosha.

     
  • Tarehe 2/11/2006 10:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Sasa anonimasi naona kiu yangu imekwisha mimi nilifikiri ni askari wa myavuli wa makene akiwa katika himaya yake.Rakini nimekaona ka Karuti na Nyamubwe Mura...Hao nao siyo mapoti?.Usimind sana mura mimi natania bwana.....

     
  • Tarehe 2/11/2006 10:51 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Hahaha!! Mwaipopo kweli we Mnyakyusa (Mtu wa Mbeya) Kwa sababu ga ga nyingii, hahaha! Huwa-ga hawana-ga. Fresh sanaa lakini unanikumbusha nyumbani. Muulize Makene a.k.a Kasri ananijua mimi ni nani a.k.a (Anangisye).

     
  • Tarehe 2/12/2006 11:34 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Hizo stori za upoti mimi simo maana matani ya UDSM siyawezi mtaalamu Anangisye nipe siku moja nadhani kesho nitakuja na nyingine ukumbuke tulikotoka.

     
  • Tarehe 2/18/2006 7:57 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    hahahahaha Mwaipopo, umenikumbusha nikiwa mwaka wa kwanza niligombea umakamu wa raisi! kikubwa ni kuwa kuna bwana mmoja rafiki yangu alikuwa Mngoreme - , aliingiza timu pia!! kibaya au kizuri zaidi alikuwa ni room mate wangu!! - nakumbuka vijana walimwomba atoe timu ili nishinde wa mteremko akawa ananifuata, akaniambia bwana mudogo, ninaomba uniachie hii nafasi halafu nitakupa uwaziri!! - tatizo sera zake hazikuwa bomba!!na pia tatizo angetoa upinzani mdogo kwa yule dada wa kiganda - alikuwa mwaka wa pili ambao walikuwa wanaungwa mkono na main campus kwani walikuwa wanahamia huko, na wimbi la gender lilikuwa ndio linakuwa hasa ukizingatia yule dada alikuwa anatisha tisha kipesa...nimesikia kaolewa na mtoto wa kabaka na sasa wako Holland! - nilikuwa wa wa pili nyuma yake na Mgoreme wa Tatu - alifanikiwa kugawa kura!!! wakati huo SUA ilikuwa chinja mtu 50 % ya frirst year lazina iondoke!!!, moja ya maswali niliulizwa ni "wewe first year ukinyakwa huoni kuwa utatuingiza gharama kuchagua makamu mwingine?- niliwahakikishia nitatoboa na nikatoboa bila kushikwa shati!!!" - maana serekali iliyopita walikula kichwa raisi!!


    unajua huyo anoni ni namba fulani inayojua sana mambo ya uendeshaji wa serekali za wanafunzi vyuo vikuu!! - mmenikumbusha mbali!!

     
  • Tarehe 2/06/2008 5:32 AM, Mtoa Maoni: Blogger MBOGELA, Jackson

    vipi Mark, Lakini nadhani kama objective amabzo tulikuwa nazo tukiwa chuo tutaendelea nazo mapak huku mitaani basi Tanzania yetu itegemee mabadailiko.

    Lakini nakumbuka hata huko vyuoni watu waliorganize migomo chini chini wakitaka kuwa anonymous, hawa sioni kam kweli walikuwa na ujasiri ambao mwakyembe na akina zitto, slaa na wengine wanonyesha bungeni

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved