Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, February 12, 2006
KUMBUKUMBU PEKEE NA KIONA MBALI

MWENYEZI kaa naye vema Kiona Mbali (Conrad Danstun) hapa alikuwa nasi Mwananchi ya wakati huo ikielekea kukamilisha mwaka mmoja. Haya Ndesanjo una mtu unamkumbuka hapo?
 
© boniphace Tarehe 2/12/2006 01:40:00 PM | Permalink |


Comments: 20


  • Tarehe 2/12/2006 8:00 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Mungu amlaze mahali pema peponi.Nilikuwa mpenzi wa uandishi wake sana.

     
  • Tarehe 2/13/2006 11:27 AM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Ndiyo yupi hapo? Maana kwenye gazeti alikuwa-ga haweka-gi kapicha kake. nakumbuka tukiwa shuleni Malangali kuliibuka waandishi wa gazeti la shule woote wakijiita Kiona Mbali. Lakini hasa rafiki yangu mmoja mchagga ndiye hatimaye akaitwa Kionambali. Hata leo nimesahau jina lake bali namkumbuka kwa jina la Kionambali.

     
  • Tarehe 2/14/2006 5:47 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    Nimemkumbuka. pamoja na Column yake ya Konambali na Baadaye maono ya Mwona Mbali, aliwahi kuwa na Mashavu Mapana na zote zilipzndwa na watu. Lakini kwa story za kawaida za mtaani alikuwa muongo sana, alikuwa anatoa zile tunaita 'fix' mfano 1., alikuwa amesevu simu ya bosi wake, Theopihil Makunga kwa jina la Mkapa. alipokuwa anapigiwa simu na bosi akiwa kwenye kundi la watu aliionyesha na kudai Mkapa anampigia...kisha anaitikia 'Halo Chief...watu wanadhani kweli ni Mkapa (rais) 2. siku zote alijiita yeye ni usalama wa Taifa..hilo sina uhakika kama alikuwa ama hakuwa.

     
  • Tarehe 2/14/2006 8:00 AM, Mtoa Maoni: Blogger Christian Bwaya

    Aisee Kasri kazi yako si mchezo. Sikuwapo mtandaoni kwa muda, nimekubali mabadiliko makubwa uliyofanya. Hili la kuweka picha ni safi sana!

     
  • Tarehe 2/14/2006 10:30 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Mwaipopo Kiona mbali yupo hapo chini akikaribiana na binti mwenye suti nyeusi na ana flana nyeupe na jinsi bluu. Huyo ndiyo ndugu yetu. Hayo ya Miruko siyafahamu vema maana watu wazima hawa.

     
  • Tarehe 2/16/2006 5:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

    Mimi nailikuwasipo, lakini nimeingia hapa na majonzi makuu kwa hii kumbukumbu ya kiona Mbali nakumbuka machozi yasiyopimika yaliyonitoka wakati tunaupeleka mwili wake pale katika makaburi ya Kinondoni,huyo alikuwa mwalimu wangu katika habari za michezo pale mwananchi, ndio nilikuwa mwananchi wakati huo. huyu ni kalamu ya mfano,nasema kwa kinwa kipana kwa kuwa wengi wamekuwa wakiiga mbinu zake za uandishi hasa katika michezo muulizeni Charles Mateso wa Burudani na Uhuru,Muulizeni Innocent Munyuku na Zena Chande, Makene nashukuru sana kwa kuweka kumbukumbu hii, lakini wakati unafanya ijitihadi ya kumleta huyu mpiga picha wetu Leah, TAFADHALI hebu jitahidi na huyu DADA mWINGINE bi Anastazia Anyimike aanze kuandika michezo humu, pia na yule Mbonile Botton wote si mpo katika kiota kimoja

     
  • Tarehe 2/16/2006 5:08 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

    hivi huyu mwingine ndio Mhariri habari siku hizi Deo Balile ama nmaana nilipokuwa mwananchi alikuwa na kijimwili finyu lakini si kama hiki, na kwa sasa atakuwa hata tai kufunga kazi

     
  • Tarehe 2/16/2006 10:03 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Nyembo nashukuru, katika picha hiyo Balile hayupo bali yupo iliyo chini yake. Sasa Balile ni Mhariri Mtendaji Tanzania Daima. Hivi ulikuwepo na wewe pale Kinondoni wakati tunampeleka kwake Kiona mbali? Sasa tazama kutojuana kubaya sana nikifika Bongo tutawasiliana na kupiga tupicha na kutuweka kwenye mburogu zetu. Ok hao wa michezo wagumu sana wananihitaji niwe nao ana kwa ana ndio wanaweza kuingia maana sasa naogopa kuhamasisha mtu kisha anaingia ukumbini kama mamluki siku mbili anakimbia.

     
  • Tarehe 2/17/2006 4:52 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

    NAKUMBUKA TULIANZIA OFISINI JENGO LA CCM, KISHA SINZA HALAFU KINONDONI KWA GARI YETU ILE YA OFISINI, INGAWA SIJUI KAMA BADO IPO PALE MAANA MIMI NIPO HUKU KWA KINA KULANGWA SIKU HIZI,LAKINI SWALI MUHIMU HAPA MALENGA MNALIKUMBUKA JINA LA CONRAD DASTAN AMA KIONA MBALI KATIKA MEDANI YA USHAIRI ALIITWA NANI?.....

     
  • Tarehe 2/17/2006 10:09 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Nyembo nikumbushe maana isije ikawa lile la Malenga wa Kamachumu. Sikumbuki sana ila najua Kiona Mbali alikuwa Malenga safi sana.

     
  • Tarehe 2/18/2006 8:42 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Kwa kweli hapa lazima nikiri kuwa Makene amefanya kazi kubwa sana kutukumbusha ndugu yetu kipenzi Conrad Danstun lakini jambo moja ambalo limenihudhunisha ni kwa huyu mwanataaluma mwenzetu Reginard Simon kutoa kumbukumbu ambazo zinaleta majonzi.

    Katika imani za dini fulani tunaambiwa kuwa iwapo mtu ametangulia mbele ya haki basi hatuna budi kumkumbuka kwa mema yake na kumuombea kwa Mola ampunguzie adhabu kutokana na yale aliyoyakosea akiwa hapa duniani.

    Wajua sote hapa duniani tuna mapungufu yetu sasa tukianza kuanikana hadharani sidhani kama kuna mtu atapenda kuonesha uso wake mbele za watu seuze kwa mtu aliyetangulia mbele ya haki?

    Namkumbuka Kionambali kwa mengi hususan katika ile safu ya KUNGA ZA KIONAMBALI, hadi sasa hakuna aliyekava ile safu.

    Nadhani kwa wakati ule Makene ulikuwa bado haujaanza kuandika mashairi ndio maana umemsahau malenga huyu mahiri katika fani,Nyembo amekumbusha kitu adhimu sana kwa upande wetu malenga, Conrard Dastun tulikuwa pia tukimfahamu kwa jila la (LUNA NOVA)ama(NGURUMO YA KAMACHUMU) hadi kifo chake sikupata kufahamu maana halisi ya jina lake hili,ni bahati mbaya sana Mungu aliamua kumchukua hata kabla kiu yetu ya kusoma mashairi yake na kunga zake katika gazeti la MWANANCHI haijakatwa.

    Natoa changamoto kwa washairi wa Blogu kabla sijaliweka bloguni shairi la (Ngurumo ya Kamachumu) atokeze mwanaume wa shoka alete japo shairi moja la Marehemu Luna Nova.

    Kazi kwenu akina Makene, Nyembo, Mwandani na wengineo mnaotumia mashairi hata kama si mshairi jitokeze na uliweke bloguni shairi moja la KIONAMBALI

    MDHAMINI WA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI WATATU WA KWANZA WATAKAOLETA SHAIRI LA MAREHEMU KIONAMBALI AMEJITOKEZA.

    WAKATABAHU

     
  • Tarehe 2/18/2006 9:37 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

    Luna Nova twakumbuka,mhenga ulotuacha,
    mitano idadi myaka,toka mungu kukuficha
    sisi tupo nawe kaka,ingawa ulitukacha,
    tuma kwangu tungo zako,zawadi nataka zipata.

    Unajua nimekumbuka mbali sana, katika picha moja hivi(No retreat No surrender)kijana ili ashinde mapambano ilimbidi aende katika kaburi la bruce lee amuombe ampe walau kaujuzi sasa kwa zawadi hii ya mkwinda inabidi nimuombe Luna Nova mwenyewe kabla ya kwenda Maktaba kuanza kusaka tambo zake

     
  • Tarehe 2/18/2006 12:07 PM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Nashukuru sana Nyembo hilo jina la LUNA NOVA naomba unisaidie tena kupata maana yake. Hili nalo tufanye ni zoezi kama kupatikana kwa mashairi yake. Ningekuwa Bongo ningeyapata lakini huku ughaibuni sijui, walai bora hizi mburogu zingekuwepo mapema ningeweza kutafuta humo na kuchukua moja.

     
  • Tarehe 2/19/2006 2:25 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

    sawa ndugu yangu nitajtahidi sana kutafuta maana halisi ya LUNA NOVA ili nipate kukujuza!

     
  • Tarehe 2/21/2006 4:07 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    Kweli Bwana Rashid Mkwanda amepatia. Conradi Dunstan Mnywambele alikuwa anajiita (LUNA NOVA)ama(NGURUMO YA KAMACHUMU)katika kunga zake. Alianza kuziandika wakati akisoma katika Seminari ya Rubya.

    Kuhusu kukumbushia 'mabaya' yake Nilifanya hivyo makusudi. Kwenye taaluma ya uandishi wa habari na maadili "ni Ethical Dillema".

    Nina maswali ya kujiuliza:
    Je,naruhusiwa kuficha ukweli?
    Je,Kipi bora kusema uongo wa kumpaka marehemu mafuta kwa mgongo wa chupa au kusema ukweli juu yake?
    Je, Asipotokea mwandishi akakuletea ukweli huu wewe utaujua kwa njia gani?
    Je, Conrad alikuwa malaika kama ambavyo wengi wanavyomuelezea sasa?

    Maswali kama haya, yaliwahi kuzua utata, pale gazeti la Washngton Post lilipotoa Tanzia (obituary) ya mwanamama mmmoja na kutaja waziwazi, kuwa aliwa ameshafikishwa mahakama mara 84 kwa makosa mbalimbali mengi yakihusiana na uzinzi. Wengi walipinga, lakini Mhariri alisisitiza kuwa alichofanya ndio kazi yake ya kuripoti ukweli.

     
  • Tarehe 3/05/2006 3:50 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    Bw. Simon, Miye naitwa Mkwinda siyo Mkwanda nadhani kulikuwa na makosa ya kuchapa, ok si mbaya ngoja nirejee katika mada ni kwamba,ni vyema kukumbusha mazuri ili iwe ibra njema kwa wengine, unapokumbusha maovu ya mtu aliyekufa ili iwe nini? kwani hawezi kuruidi kujirekebisha alichotakiwa kufanya Bw. Simon enzi zile za uhai wa marehemu ni kumuonya aachane na uongo sasa amengojea ameiaga dunia anaanza kumteta kwa kweli mie binafsi sijafurahia kitendo hicho, watu hivi sasa tunadiriki kuwateta hata maiti, hivi Bw. Simon alikuwa wapi kumueleza mwenyewe akiwa hai ajirekebishe tabia yake.

    Kwanza kuna haja gani ya kuyajua mabaya ya marehemu?unajua kuna watu waliokuwa karibu na marehemu ambao walikuwa wanakubali kazi zake,wanaweza kudhani kuwa asili ya mafanikio yake yametokana na uongo hivyo wanaweza kuiga uongo, itakuwa ni kujenga ama kubomoa? jamani tukumbuke mema ya wale waliotutangulia, mabaya tuwaachie wenyewe wakapambane na mola wao kaburini.

     
  • Tarehe 3/05/2006 10:42 PM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    bwana mkwinda nashukuru. Nionavyo mimi 'kama hakuna sababu ya kuyajua mabaya ya marehemu, pia hakuna sababu ya kuyajua mazuri yake'. Period.

     
  • Tarehe 3/16/2006 1:51 AM, Mtoa Maoni: Blogger Rashid Mkwinda

    No! Bw.Simon,tunakumbuka mema yake ili tupate kujifunza kwayo mabaya si mema maigizo,mazuri ndiyo tujivuniayo na kujinaki kwayo, lakini kwanini tuyakumbuke mabaya.

     
  • Tarehe 3/18/2006 12:19 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Heri yule aliyebuni jambo hili. Nimeguswa na maoni ya wengi juu ya Conrad Dunstan. Mimi sitasema mabaya yake kwani kama yalikuwapo basi ni udhaifu wa kila binadamu. Binafsi Conrad Dunstan licha ya kuwa sahiba wangu wa karibu namkumbuka kama mwalimu katika mambo mbalimbali ya taaluma hii ya uandishi wa habari. Nimekuwa karibu naye tangu mwaka 1997 na baadaye akaja kuwa bosi wangu katika dawati la michezo kuanzia 2000 hadi mauti yalipomkuta Februari 2003. Hakuwa mwenye hiyana na wala hakuna siku nimemsikia akifura kwa hasira hata pale niliposhindwa kuwajibika vema alinielekeza kwa hekima. Nakumbuka pia jinsi tulivyoambatana katika sehemu nyingi za burudani na katika hili sisiti kusema kuwa aliipenda sana Twanga Pepeta wakati huo ikivuma kwenye Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni. Lakini katika kupenda kwake muziki alipenda utani. Kwa mfano alipata kuniambia 'Innocent ukitaka kuwajua watu waliopo ukumbini huna budi kukaa jirani na njia ya msalani' Niliishia kucheka. Daima nitamkumbuka Conrad.

     
  • Tarehe 1/15/2011 9:39 PM, Mtoa Maoni: Blogger Joseph Zablon

    Conrad Munywambele, jina lake katika uga wa mashairi alijiita Ngurumo za Kamachumu, kikubwa ambacho sitakisahau ni tabia yake ya kubeba lawama na makosa ya wengine katika chumba cha habari hasa kunapokuwa na hali ya makundi na utengano...!
    Nakumbuka kuna siku ripoti mmoja alibanwa na wenzake wakati wa postmorterm kuhusiana na stori ambayo alishindwa kuipata na kudai kuwa alielezwa sivyo na mmoja wa wahariri lakini wenzake wakawa wakali na kumlazimisha amtaje na kwa kuwa Luna Nova alijua kuna kukamiana kwa wadada hao, aliingilia kati na kudai ni yeye ndie ambaye alimpotosha ripota huyo, kesi ikaisha..!~

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved