
HII ndiyo Mkwawa, Chuo kilichogeuzwa Sekondari ya Juu pekee Tanzania. Sasa hivi imerejeshwa kuwa sehemu ya Chuo Kikuu Dar es Salaam. Tazameni panapendeza hapo Baragumu nadhani utakuwa na kazi ya kutembelea hapo. Panaanza chuo kikuu mwaka huu wa masomo unaoanza Septemba.
Heri kwani nafasi za ajira ya kudurusu vyuoni yapanuka. Tena Karibu na nyumbani Mbeya. Hakuna joto wala foleni za daladala Kama Da'Slam. Cha muhimu ni kukaza misuli darasani katika miaka hii ya usoni ili kumakinika katika fani.