GAZETI moja la Kiingereza nchini Tanzania limechapisha habari juu ya Waziri mpya wa Ulinzi Purofesa Juma Kapuya kutumia dege la jeshi katika safari zake binafsi kwenda kwao Tabora. Tukio hilo limeisababishia wizara hasara ya zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 10. Waweza soma habari hii zaidi hapa na kutoa maoni yako.
Kumbuka tu nchini Kenya kuna wimbi la matumizi ya fedha za serikali visivyo ambalo sasa napo limezaa kujiuzuru kwa Waziri wa fedha kama inavyofafanuliwa zaidi hapa.
Hahah!! Kaka Makene. Watu wanalalamika kuna njaa, mtu anakwenda na ndege kusalimia,Si bora angebeba na chakula na kudondosha kwa wenye njaa. Hivi waziri kama huyo anawaza kwamba kuna wananchi wanakufa njaa kweli!! (Binadamu wote ni sawa na Afrika ni Moja) Yeah right!!