Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, February 18, 2006
JINA LA KISWAHILI LA BLOGU
MJADALA wa kupata jina la Blogu kwa Kiswahili chetu umepoteza muelekeo! Samahani kwa kuanza hivi maana naweza kuonekana mvivu wa shukrani kwa waliojadili. Sasa nashambulia tena maana kumbuka tulikotoka na kupata neno blogu. "Blogspot" Ndesanjo wiki mbili zilizopita amehama huku na kuingia "wordpress." Hii ni mitandao miwili tofauti inayotoa huduma moja. Nakumbuka namna Mobitel walivyoingia Tanzania na simu za mkononi zikaanza kuitwa mobitel. Ilichukua muda kufuta jina hilo hadi walipoingia VODACOM na Celtel. Sina lengo la kujadili makampuni ya simu mathalani Vodacom na hatma ya Msekwa! Sina habari kabisa kuhusu kusitishwa kwa ajira yake ya uenyekiti wa Bodi hiyo na wala sina uhakika kuwa Mkapa naye ana hisa nyingi katika kampuni hilo.

Makala yangu ni kutafuta jina la Blogu ili watakaokuwa Blogger au wordpress au ile ya Mike Mushi wa Tanzania na nyingine nyingi zijazo wawe na jina lao la Kiswahili. Hawa Blogger, wordpress na wengineo wabakie kuwa kama viwanda vya kuchapishia magazeti yetu tu. Ok naishia hapa na kuomba neno la GAZETI TANDO kuanza kutamalaki.

Wasalaam,
 
© boniphace Tarehe 2/18/2006 02:24:00 PM | Permalink |


Comments: 11


 • Tarehe 2/18/2006 3:42 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Makene nadhani jina au neno gazeti tando ndio liwe muafaka kwa hivi sasa.Naunga mkono kulipitisha na pengine kuanza kulitumia.Tusiwe kama wanasiasa,linalowezekana leo lisingoje kesho waungwana.

   
 • Tarehe 2/18/2006 9:22 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

  Kasri uko fiti kwa kutohowa maneno!Naaminia mwanangu.Mimi nakuunga vyote kuanzia kichwa, mikono hadi miguu isipokuwa tu ki.....na mgo....

   
 • Tarehe 2/19/2006 1:37 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Nikiwa naunga hoja ya kutafuta neno la kiswahili, nakupinga kuwa tumekuwa tukitumia 'blogu' kutokana na 'bogger'. Hawa blogger.com wamechukua advantage ya maana ya 'machapisho binafsi huria'. Kwa maana hii hata hao wa wordpress nao wanablogu tu (They still 'blog') Hata wa Mike Mushi nao wana-'blog'. Mfano wako wa Mobitel, Tritel, Vodacom nk hauswihi hapa. Kublog manaake kuchapisha huria mtandaoni, iwe kutumia kampuni yoyote iwayo inayotoa huduma hii. Tazama neno blog kwenye kamusi yoyote ya Kizungu uliyonayo.Kuwa na blogu yako hakuna maana yoyote ya kutumia blogger.com pekee

   
 • Tarehe 2/19/2006 1:45 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

  We Mwaipopo acha hizo sisi tunataka neno na sio mjadala maana mijadala kama hii imetufikisha hapa na sasa hatuna neno badala yake tunatatarika tu kama walevi wa keroro

   
 • Tarehe 2/19/2006 11:37 PM, Mtoa Maoni: Blogger mwandani

  pigeni kura, muwache ubishi

   
 • Tarehe 2/20/2006 6:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

  Ahsante Mwandani sasa tunakoelekea ni kwenye ubishi!
  Mimi sipendi hulka ya kuunga mkono hoja katika utafutaji wa jambo muhimu kama hili, bado hatujashindwa kupata maneno muafaka kwa uteuzi wa nen hilo tumiko linalotarajiwa, naomba sasa turudi katika quicktopic na kuchagua maneno muafaka na kisha kuyapigia kura bila kutumia ushabiki, kwa kuwa tukiweka ushabiki hakika tutaipoteza jamii husika itakayotumia neno hilo....naona neno muafaka kwa kulitumia ni TANDOPEPE
  ALAMSIKI

   
 • Tarehe 2/20/2006 6:31 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Kasri asante sana kwa kutukumbusha. Najua watu bado tuna nia ila tunakuwa tumetingwa na kukamatwa huku na kule.

  Nitapenda kuandika usiku kirefu maoni yangu juu ya maneno ambayo yamependekezwa. Ila kwa sasa nitapenda kukubaliana na Mwaipopo kuwa neno blogu halikutokana na huduma ya jamaa wa blogger/blogspot. Huduma za blogger, wordpress, livejournal, typepad, n.k. zote ni huduma za blogu. Jamaa wa blogger waliamua kutumia neno "blog" kuweza kutangaza huduma yao lakini hili neno sio lao na wala hawakuanzisha wao. Neno hili ni ufupisho wa neno la awali ambalo ni "weblog." Kwahiyo anayetumia blogger, anayetumia wordpress, anayetumia typepad, anayetumia livejournal wote ni wanablogu kwahiyo hakutakuwa na haja ya kutafuta jina kwa kila huduma tunazotumia. Fani ina jina moja, ila huduma tunazotumia zina majina mengi.

   
 • Tarehe 2/20/2006 7:31 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Sidhani kuwa kuna kosa kwa Mwaipopo kuendeleza mjadala. Jambo tunalozungumzia ni jipya hivyo kuna mengi ya kufunzana, kuwekana sawa ili tufikie makubaliano. Ni vyema kufikia makubaliano mapema ila hakuna sababu ya kukimbizana maana mjadala huu wa neno hautuzuii kuendelea kufaidi matunda ya teknolojia yenyewe. Tusiwe kama serikali zinavyopenda kupitisha miswada bungeni haraka haraka bila majadiliano kwa mapana na marefu. Mimi namshukuru Kasri kwa kutuamsha. Nadhani safari hii tuamue kutilia maanani. Kama nilivyoahidi hapo juu nitaandika maoni yangu juu ya maneno ambayo tumeyatoa.

   
 • Tarehe 2/22/2006 6:46 AM, Mtoa Maoni: Blogger Michuzi

  hata vituo vya mafuta twaviita sheli, na soko la samaki magoni ni feri, au hujasikia bustani ya mnazi mmoja garden. anyway, naomba maoni yangu kule quicktopic yatazamwe...ili, kama nyembo alivyosema, isije kuwa zogo

   
 • Tarehe 2/24/2006 5:37 AM, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

  kwa sababu muda mrefu umeishapita na jina mwafaka limekuwa halipatikani kwani jina blogu limekuwa linafunika jitihadi zetu. naunga mkono hoja ya Makene kuziita hizi mambo zote jina moja iwe world press (ambayo nashindwa kutoa maoni) au blogu! historia inaonyesha kuwa jina hutumika isivyo hadi ikajulikana maana halisi. nani alijua Hayati maana yake ni ALIYE HAI? nani alijua kuwa UKWASI ilikuwa inatumika ilivyo na ni kinyume na UKATA?

  nikisema hivyo naomBa kutoa hoja! GAZETI TANDO ITUMIKE RASMI KUANZIA LEO NA JINA MAHUSUSI ZAIDI LITAPOTOKEA LITAJADILIWA NA KUANGALIWA KUPITISHWA!

   
 • Tarehe 3/09/2006 8:06 AM, Mtoa Maoni: Anonymous ndesanjo

  Michuzi kanikumbusha jambo nikacheka sana. Kule moshi bado tunaita vituo vya mafura sheli au agipu. Barabara ya lami, au mjini kwa ujumla tunaita stelingi (yaani steering = usukani). Na magari yote madogo zamani tulikuwa tukiyaita pijo au teksi.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved