Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, February 02, 2006
HEKIMA ZA KASRI ZAANZA KUNUKULIWA
SI kazi rahisi maandishi yako kutumika na wengine kama hayana weledi na urazini. Ni lazima utoe hoja sawia na yakinifu ili uweze kunukuliwa. Katika kuonesha kutanuka kwa mawazo na fikra za wanablogu ndipo kaulimbiu ya Kasri ilivyokutwa ikinukuliwa katika habari hii na Mwanablogu maarufu kutoka katika hatihati na harakati za wanavyuo wa Tanzania. Kunukuliwa na Mwanazuo ni kuonyesha namna mawazo yako yanavyokuwa na kuthaminika.
 
© boniphace Tarehe 2/02/2006 11:25:00 AM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 2/02/2006 12:00 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Kuweza kunukuliwa kwaonyesha walau kuna mtu au jamii inayokiri nafasi yako katika mawazo pevu.

  Nimeoa mwanamke mwingine. Yule wa zamani hanitaki asilani ingawaje nampenda.Huyu wa sasa anaitwa: mwaipopo.blogspot.com Nawe waweza kumbadilisha pale kwenye kiunganishi chako.

   
 • Tarehe 2/02/2006 5:21 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jacob Lubuva

  Kaka Makene, nashukuru sana kwa kazi nzito uliyoifanya kwa kumtangaza mwali JARIDA LA UGHAIBUNI. Si mchezo mwanangu nimetembelewa na watu saba, nami nimefarijika sana, kwa sababu si tu watu wanahamu na mawazo yangu, bali ni uwanja wa kujuana na watu na kupata marafiki toka sehemu mbalimbali za Dunia pia.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved