Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, February 03, 2006
ELIMU INAPOGEUZWA KIFUNGO


MABANGO haya nimeyakuta Chuo Kikuu cha Carleton pale Ottawa, Canada. Nilichukua picha hii kukumbukia vita inayokuja Tanzania baada ya kuundwa kwa bodi ya mikopo inayodai malipo ya masomo vyuo vya juu kwa wanafunzi kuanzia mwaka 1994. Kumbuka kuwa elimu hiyo ilitolewa burew kabisa tangu huko nyuma na nini hasa kimeleta hoja ya madai kuanzia mwaka 1994 au kwa kuwa kundi hilo halikuwa na wawakilishi katika Bunge? Kwa nini madai ya kusomea fedha za serikali yasiwahusu wote waliowahi kupata fedha hizo na ukweli wanafahamika. Kwa sasa wakati ambapo kazi zimekuwa adimu elimu inageuzwa kuwa kifungo, tazama picha hizi huku ni nchi zilizoendelea na vipi nafasi ya Tanzania.
 
© boniphace Tarehe 2/03/2006 11:30:00 AM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 2/03/2006 5:03 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Kifungo kinachoongelewa hapa Canada kupitia mikopo ya elimu sio sawa na kile cha Dar-es-salaam.Hapa linaongelewa suala la unafuu wa mikopo ili mwanafunzi anapomaliza asiwe na kibarua cha kufanyia kazi serikali ili alipe deni.Kama sikosei pale Dar kilichokuwa kinadaiwa ni kwamba wote wadaiwe la sivyo na sisi tuendelee kusomeshwa bure!Nadhani pale wasomi wetu walikuwa na hoja ya msingi lakini wakashindwa kugundua kwamba ofisi zetu za takwimu zimejaa vumbi tu.Utawajuaje wadaiwa wa zamani?

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved