Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, February 01, 2006
BLOGU ZATANGAZWA KUWA HAKI YA MSINGI KWA KILA MTANZANIA: TATU ZAFUNGULIWA KWA SIKU MOJA
KAMA ndoto vile ndivyo tamko rasmi lilivyotangaza sasa. Lisome hapa kuhusu haki ya msingi kwa raia wa Tanzania sasa kumiliki Blogu lake. Wakati nikitembea nikawa wayani (katika mazungumzo ya simu) na Baragumu. Mazungumzo hayo yakazua neno na mjadala kuhusu ughaibuni. Ikawa kama tulikuwa tunaota kelele zetu za kuhamasisha blogu jipya kufunguliwa kule Stanford, California. Usiku wakati tukiwa katika mazungumzo ya kukaribisha blogu hilo jipya akaja huyu jamaa akahamasishwa kufungua Blogu kwa maelekezo ya simu akiwa KASRI na Baragumu na kisha Jarida la Ughaibuni akitumika kutuunganisha kwa simu yake. Baada ya dakika kama kumi na tano ikafunguliwa hii inayoitwa Kisima cha Weledi kutoka katika jimbo la Barrack Obama, mkenya yule Seneta wa Illinois. Baada ya hapo kama haitoshi kwa siku hiyo nikakutana na kijana wangu wa siku nyingi Gadiel kutoka nyumbani naye akinitaarifu kuwa harakati za kumuhamasisha sasa zimetimiza jukumu na blogu lake jipya hili hapa limefunguliwa. Kumbuka katika mwezi huu kuna blogu zaidi ya tano ambazo zimefunguliwa kwa mtindo wa papo kwa papo.

Nadhani jitihada hizi zafaa kuigwa na kupongezwa na hasa ndugu Jikomboe kwa ukarimu wa kukaribisha wanablogu wapya. Nitoe rai tu kwa wanablogu wapya, Kumbukeni kupita kwa wenzenu na kuwasalimia ili nao wapite katika majumba yenu. Na wanablogu wakongwe wasio na tabia ya kupita kwa wenzao wawe macho watakimbiwa maana mburogu sasa zimetangazwa kuwa haki ya kila raia Tanzania!
 
© boniphace Tarehe 2/01/2006 09:27:00 AM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 2/01/2006 10:04 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Keleuwii...ngoja nilipige mayowe ya Kichagga kabisa. Ruwa oko!
  Safi sana kazi mnayofanya kutuletea hawa ndugu. Ngoja niwatembelee na pia kuwatangaza.

   
 • Tarehe 2/02/2006 2:35 AM, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

  kaka makene, kwa kweli hii imekuwa ni kama mapinduzi...yaani kama ni bastolka ni revolver...

  lakini makene kitu kimoja, kiunganishi cha jina lako unapochangia mada kwa wenzio huwa hakituleti kwako moja kwa moja? unakumbuka kuna siku nilikuhimiza uanze kuweka makala? hapa nimekupata kupitia kiungo pale kwa Jeff....

  naamini kuwa wengi tulikuwa tunakutafuta tukakukosa......

  ninachofanya hapa SA tuna email group adress yetu ya yahoo, huwa nawawekea viongo wasome habari za wanablogu na kuwahimiza wajiunge...wanazipenda, lakini naamini hata wewe umeona kuwa ushawishi huchukua muda kidogo lakini wataiva tu penda wasipende...unajua tuliopata shida tulikuwa sisi ambao tulikwa na maoni bila kujua kuna kitu yaitwa blogu? wao wanajua teyari, ni muda tu haujafika - ni time bomb!

  haya ni mapinduzi....sasa wewe ni waziri mkuu wa blogu!

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved