Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, February 23, 2006
BLOGU YA PICHA NYINGINE HIYOOO
BARAGUMU kanitumia ujumbe ambao ukanipa furaha na kicheko cha namna nilivyo nyuma ya wakati. Ni jana tu nilipata jina hili mtandaoni kisha nikaona nimuandikie ujumbe ili kumtaka aje kwenye ukumbi huu. Kuamka leo nagundua kuwa yumo na ameiva kisawasawa. Haya ni mapinduzi ya kasi kwelikweli yatembeleeni na kuyasabahi.
 
© boniphace Tarehe 2/23/2006 03:47:00 PM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved