Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, February 12, 2006
ANA KWA ANA NA NGASONGWA

KASRI siku moja alikutana na swali gumu toka kwa Waziri Ngasongwa. Hili lilitokana na utambulisho toka kwa Profesa Mbago pale alipomueleza Ngasongwa kuwa Kasri ni Waziri Mkuu wa DARUSO. Ngasongwa akawahi na kunisalimu, "Habari yako Waziri Mkuu" nikacheka...sikutoa jibu mapema. Ungekuwa wewe ungemjibu sijambo mheshimiwa Waziri au vipi ukikumbuka kuwa kwake yeye Waziri Mkuu ni alikuwa Sumaye?
 
© boniphace Tarehe 2/12/2006 01:15:00 PM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved