PICHA hii nadhani ingekuwa muwali sana kutumika kwa
Damija maana yeye maudhui ya Gazeti Tando lake linajadili haya. Lakini hata katika KASRI suala la haki za jinsia zote hupewa kipaumbele na kuthaminiwa. Hapa hakuna unyonyaji na wala hakuna kuangalia unyanyasaji na udhalilishaji unapewa mianya katika jamii. Picha hii pia niliipata pale Carleton na niliichukua kwa hisani ya wasomaji wa Kasri la Mwanazuo.
Nakumbuka bwana Nyembo alishawahi kusema kwa bwana Mkwinda "mwanzo wa moto ni cheche, hivyo apokee cheche ili azibariki ziwe moto"
Na mimi Da'Mija ninasema, Makene na wanaume wengine duniani pokeeni cheche hizo na mzibariki kuwa moto. Hao wachache wameanza na nyie wengine malizieni.
Tupo pamoja.