Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, January 03, 2006
WANDUNGU NIMEMLETA WAZIRI MKUU MUMTAZAME


MOJA ya matukio nitakayoyakumbuka katuka kuumaliza mwaka na kuanmza huu ni kukutana na mheshimiwa Jeff Msangi na kulishana fikra. Makutano yetu yalianza hivyo na mengi nimeanza kuyaandika na kuyatuma nyumbani ili wasomaji wa huko wanufaike pia. Kumuona Jeff si faraja katika kizazi cha Blogu za Tanzania bali mwamko mpya wa safari kali ya kukuza na kuujengea heshima uwanja huu. Nadhani mwaweza hapo Bongo Miruko kumtembelea Michuzi ama Materu. Kutoka Texas hadi Toronto si mchezo lakini inawezekana kama tutatambua kuwa umoja huu ni sawa na ule tuliozoea wa watuma salamu katika redio na magazeti
 
© boniphace Tarehe 1/03/2006 07:22:00 PM | Permalink |


Comments: 8


 • Tarehe 1/04/2006 1:16 AM, Mtoa Maoni: Blogger Phabian

  Ninashukuru kwa kutukumbuka kwamba sisi pia tunahitaji kumwona bwana waziri.katika mila na desturi zetu kutembeleana kwa marafiki na wanandugu ni moja ya nguzo katika maadili ya mwafrika .

   
 • Tarehe 1/04/2006 4:18 AM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

  Kaka makene!waziri mkuu huyu ndiye alishirikiana na mheshimiwa kikwete katika kumfanya mzee kingunge askari kamili wa miavuli(FULL MINISTER)??????

   
 • Tarehe 1/04/2006 7:07 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Materu nimepata baraza la mawaziri zima sasa na kiasi fulani kuna mambo ya kucheka moja ikiwa hilo na la pili la kumuandaa kijana wa Mwiunyi kuongoza Tanzania na Zanzibar.

   
 • Tarehe 1/04/2006 10:10 PM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

  Hili la Hussein mwinyi ndo la kusikitikia kwani watu wanasema wameletewa/kupandikiziwa tu mtu katika jimbo lao la Kwahani ambaye uhalisia wa maisha ya wakazi wa hapo hana historia nayo lakini kama mjuavyo wanandugu UNGUJA lazima atawale mwana chama tawala basi wananchi nao wakahadaika katika upande huo wa UMWENZAO.

  Sasa tusubiri 2010 kamati kuu ya chama itakavyompitisha kwa kishindo kugombea urais wa Zanzibar kama si muungano 2015.

   
 • Tarehe 1/05/2006 2:38 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

  Kumbe unamzidi waziri mkuu urefu?

   
 • Tarehe 1/06/2006 3:47 AM, Mtoa Maoni: Blogger mloyi

  Ulifika mpaka Toronto? Nimeona picha, duu! kumbe hata huko wanaweka viraka kwenye sakafu za vibaraza?
  Waziri huyo ataweza kusimamia wawekezaji kiufanisi ili sisi tusilalamike?

   
 • Tarehe 1/07/2006 9:45 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Nimeamini kweli mmekutana (iwapo hizo picha hamjaziunganisha!).

   
 • Tarehe 1/08/2006 1:06 PM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Ndesanjo bado picha tu ya mdogo wako ambayo nitakutumia siku si nyingi maana nimeshaiweka kwenbye CD. Wewe ulipiga na simu na tena unahoji kama tumebandika picha? Ina maana Michuzi ile picha yake na Kikwete kabandika (natania hapa)
  Majadiliano yetu nimeanza kutulia tangu kufika hapa jana lakini sina miundo mbinu ya kuanzia hivyo msiwe na hofu naweleteani kila kitu.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved